KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI) SEHEMU YA KUMI NA SABA
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA SITA: “samahani afande, lakini yule kijana mtekaji, yupo na huyo binti, wanaweza kumshambulia na yeye” aliisema Mapombeka, ambae yeye na askari wake, awakujuwa kinacho endelea, hapo sajent Kibabu aka mkazia macho ya ukari koplo Mapombeka, kisha aka mwambia, “fwata maelekezo koplo” alisema Kibabu kisha akageuka na kuwatazama askari wote waliokuwa wanawatazama, “ingia ndani ya pori, akikiisheni msako mkari unafanyika, kibari cha kupiga risasi kimetolewa” alisema Kibabu na hapo askarai polisi wakavamia pori kwa fujo, endelea.........
Nakutawanyika, wakijigawa makundi, ya watu wa nne mapaka sita, wakitembea kwa kufwatana yani kwa mstari mmoja, wanajeshi wanaita single file, msitu ulikuwa na hali flani ya miti mirefu iliyo nyooka, ya kupandwa, mala nyingi utumika kwa ajili ya mbao, nyasi zilikuwa fupi usawa magoti, zilizo wafanya watu hawa wakimbie kimbie kwa mwendo mfupi na kuanza kutembea, wengine wakiwa kushoto wengine kati kati, na wengine kulia, wote wakisonga mbele kuwasaka wakina Edgar, ukiachilia kujigawa makundi pia makundi haya yali changanya askari, yani wale wa sajent Kibabu toka Songea, na hawa wa Koplo Mapombeka wa Makambako.
constable Charles alikuwa kundi la upande wa kulia, pamoja moja na polisi watatu wa hapa Makambako, walitembea kwa haraka haraka huku wakipepesa macho huku na huku, kama wange bahatika kuwaona wakina Edgar,
Nikweli juhudi zao zikaanza kuonyesha mafanikio, maana waliona alama ya nyasi zilizo lazwa, ikionyesha kuwa kunawatu wame pita muda siyo mrefu, “wamepita huku tuongeze mwndo haraka” alisema PC Charles na wote wakaanza kukimbia kuelekea kule ambako walihisi Edgar na Monalisa wamekimbilia, *******
Rehema alifika nyumbani kwake, na kufungua duka lake la dawa baridi, lakini kichwani mwake alikuwa ana jiuliza maswali mengi sana, ambayo yali muumiza kichwa na kumnyima raha, swali la kwanza ni juu ya hisia zake za kuwa wale vijana wawili kama wana usiana na tukio la Lukas, na kilicho muumiza kichwa ni kwanini akuwaficha ndani mwake, kisha ampigie simu shemeji yake bwana Kisona, lakini baada ya kuwaza sana akapata jibu, hapo hapo akainua simu yake na kupiga nyumbani kwa rafiki yake Elizaabeth Leonard, na bahati nzuri ilikuwa ni jumamosi, siku ambayo doctor huyu bingwa wa maswala ya uzazi kwa wakina mama na wakina baba, uwa anakuwa nyumbani, “niambie rehema kuna lolote huko, maana baba doto ajalala usiku kucha ana waza juu hilo” aliongea Eliza baada ya kutambua kuwa anaongea na rafiki yake Rehema, “nahisi kuna jambo natakiwa kumjulisha, kwani yeye yupo karibu hapo?” aliuliza Rehema, “ametoka mapema sana, nazani anafwatilia swala hilo hilo, kama kuna lolote niambie nita mweleza” alisema Eliza mke wa bwana Kisona, mrembo anae ifahamu kazi pevu ya bwana kisona kwenye maswala ya hovyo hovyo kama haya,
Rehama akamweleza rafiki yake Eliza kama ilivyo kuwa tokea usiku wale vijana wawili walipo kuja dukani kwake, na jinsi walivyopishana na polisi, waliokuwa wanawatafuta, na ata asubuhi alipo amua kuwatoa nje ya mji, baada ya kuona matangazo ya kutafutwa kwa kijana wakiume, ambae alikuwa na yule binti, ambae polisi wanasema ame mteka nyala, “kama kuna lolote nita ppiga baadae na kama ata itaitaji kujuwa jambo basi mwambie anipigie” alimaliza kuongea bi Rehema Haule, mwenyeji wa Mfaranyaki Songea, ambae yupo Makambako katika kutafuta maisha.
Baada ya kukata simu, Eliza alipiga simu ya ofisini kwa mume wake, lakini akaambiwa kuwa mume wake hakuwepo ofisini, kahaidi kupiga baadae, na yeye akiacha maagizo kuwa akija ampigie.*****
Edgar na Monalisa hawakuweza kukimbia mbali, ata hii kilomita moja waliyo kimbia, ilikuwa ni kwa sababu Edgar alikuwa ameushika mkono wa Monalisa, “Eddy! me nimechoka” alisema Monalisa ambae alikuwa anahema juu juu, akionekana kutawaliliwa na uoga mwingi, huku ana simama na kuachia mkono wa Edgar kisha ana jishika kwenye magoti, maana yake aliinama kidogo, “Mona utakiwi kuchoka, hapa tusipo kimbia tutakufa” alisema Edgar kwa sauti ya kusisitiza lakini siyo ya ukali, ni sauti iliyo mbembeleza Monalisa, “tupumzike kidogo Eddy, nimechoka sana, miguu itaniuma kama jana” alisema Monalisa huku ana mtazama Edgar, aliekuwa amesimama pembeni yake, ukweli nikama Monalisa alikuwa anafanya masihara, yaliyo mchukiza Edgar, lakini ndivyo ukweli uliivyo, Monalisa alikuwa amechoka, akuwai kukimbia kimbia kama vile, tena toka jana usiku mwendo wake ulikuwa ni wa kama mbwa, ni wa kukimbia tu!, “Mona inabidi tuchague moja” alisema Edgar, kwasauti flani hiyo na utani wala ya kubembeleza tena, Monalisa alimwona Edgar nikama alikuwa amechukia, “Eddy naomba usiniache” alisema Monalisa, kwa sauti ya tafadhari, huku anasimama vizuri na kuuushika mkono wa Edgar, ambae alimtazama kidogo, kisha nikama alipoa flani hivi, akajitoa mkono wake kwa Monalisa na kumshika yeye, “sijawai kukuacha na siwezi kukuacha, lakini lazima tuchague maisha na siyo kifo” alisema Edgar, ambae alionekana kuwa bado yupo vizuri, maana yake ajachoka, nahii ni kutokana na mazoezi ya mpira wa kikap anayo fanya mala kwa mala, alipo maliza kusema hayo, Edgar akatazama huku na huku, kama anatafuta uelekeo, hali ilikuwa ile il ya baridi, lakini ukungu ulitanda angani, kihasi kwamba ata jua alikuonekana, “tuondoke” Edgar alimwambia Monalisa, ambae alikuwa ameganda, anamtazama Edgar, huku akiyatafakari maneno ya rafiki yake wa zamani.
Ile wawili hawa wanaanza kutembea tu, ghafla wakasikia “wale kuleeeee” wote wakageuka nyuma, naam kwa macho yao waka waona polisi wanne wakiwa umbali wa mia kama mia na nusu hivi, wakijawafwata mbio mbio, huku wanainuwa bundukizao tayari kuwa miminia risasi, nao wakina Edgar awakushangaa, wakaanza kukimbia mbele, huku Edgar ame ushika mkono wa Monalisa, alie valia jaket, kubwa la Edgar, lakini awakufika mbali Monalisa akajikwaa kwenye gogo la mti wa mbao lililo kuwa lime lalachini, akaponyoaka kwenyemkono wa Edgar na kijibwaga chini, mbele ya lile gogo, huku Edgar akikimbia hatua kadhaa mbele, ikifwatia mvua ya risasi na miripuko yake, “usiinuke lala hapo hapo” alipiga kelele Edgar, ambae nae alijibanza kwenye mti mmoja wapo, kati ya mingi ya shamba lile, Eddy usiniache” ilikuwa sauti ya nusu kilio ya mwana dada Monalisa, Edgar aliisikia sauti ile, japo milindimo ya risasi ilikuwa mingi, “sikuachi tulia hapo hapo” alisema Edgar kisha akachungulia kule alikokuwepo Monalisa, ambapo ndio usawa ambao polisi wale walio valia sale zao za kazi, walikuwa wanatokea,
Edgar alimwona Monarisa akiwa amelala mbele ya gogo lile ambalo lilikuwa lina pukuchuliwa na risasi za SMG, na kuanza kumegeka, ikiashiria muda wowote Monalisa ana onja utamu wa risasi, za polisi hawa ambao nao wali shambulia na kusogelea pale alipo lala Monalisa, na walikuwa wame bakiza miza chache kumfikia, “Eddyy” alipiga kelele Monalisa, kwa sauti iliyo kata tamaha, ikiambatana na kilio, huku bado risasi zikizidi kuchimbua lile gogo, sauti ya monalisa ili uchoma moyo wa Edgar, siyo kwamba alikuwa na mpango wa kumwacha, hapana, ila nikama kunakitu alikuwa ana kitegea, maana Edgar alipeleka mkono wake kiunoni na kuinua tishet lake, akaichomoa bastora, (nazani mdau ujasahau kuwa, Edgar alikuwa na bastora aliyo ichukuwa kule hotelini, baada ya kuwazidi maharifa wale polisi), Edgar aka ikoki ile bastora, na kufungua kiwamba sauti, alafu akatulia kama vile kuna kitu alikuwa ana subiri.
Nikweli milio ya risasi ikakoma ghafla, ikonyesha wale polisi walio mkaribia Monalisa, waliishiwa risasi, na sasa walianza kuangaika kutoa mazine tupu ilikupakia zenye risasi, nazani Edgar alitarajia kuwa kita tokea kitu kama hiki, maana hapo hapo ali jitokeza toka kwenye maficho, (cover) yake ya mti, huku bastora ame itanguliza mbele, akiwa ameishika vyema kabisa kwa mikono miwili, huku amfumba jicho la kushoto, ikafwatia milipuko miwili iliyo achiana nukata chache, ndani ya sekunde moja, kama vile ilikuwa utani, milipuko hiyo ya bastora ya Edgar, iliambatana na mianguko ya polisi wawili, waliokuwa busy na kubadirisha magazine za risasi, kwenye bundu kizao, “haaaaaaa” walilalamika wale polisi huku wakishikilia miguu yao iliyo kuwa ina vujadam,
“Kimbieni jamani anasilaha huyo” alipayuka Charles, nikama hawakutarajia, kitendo kile, Charles na polisi mmoja alie bakia wali timua mbio kurudi walikotokea, huku wakishindwa kuendelea kubadiri magazine kwenye bunduki zao, Edgar nae hakuacha kuwasindikiza kwa risasi kama tatu hivi, huku anawakimbilia wale polisi ambao walikuwa wame anguka chini wakitengana na bundu kizao, wakati huo Monalisa alikuwa anainuka toka pale chini, akamtazama Edgar, ambae alikuwa ana okota magazine huku akikagua zile ambazo zilikuwa na risasi, alafu akachukuwa bunduki moja, kati ya mbili za wale polisi, akaipachika magazine, na kuikoki, alafu aka waasogelea wale polisi, huku ile magazine ya pili akiiweka kwenye kiuno chake kama alivyo iweka bastora, “tafadhari usituue” alisema mmoja wapolisi wale, ambao walikuwa wanavuja damu miguuni, waswahili wanaita ugokoni, yani chini ya goti, “sikutaka kuwauwa, ila nilitaka mkawaambie wenzenu, kuwa sisi siyo majambazi, wasiendelee kutufwata, sababu nimepata SMG” alisema Edgar, kisha akawaacha wale askari na kumsogelea, Monalisa aliekuwa amesimama anajikagua, kama kunasehemu aliumia, “vipi umeumia” aliuliza Edgar, “hapana sijaumia, Eddy tuondoke watarudi wale waliokimbia” alisema Monalisa, akionyesha kuto kupaamini kabisa mahali pale, hapo wakaanza kuondokazao huku wakisindikizwa na macho ya wale askari polisi walio vinjwa miguu, kwa risasi. *****
Nikweli wazo la Monalisa lilikuwa sahihi, kumbe mashambulizi ya risasi yaliwafikia polisi wote waliokuwa ndani ya msitu ule, na waliokuwa karibu na pale ni wakina sajent Idd Kibabu, na askari wake watatu mmoja akiwa kutoka makambako na wawili aliotokanao Songea, waka kimbilia upande ule uliotokea milipuko ya risasi, ambapo walikutana na Charles na Askari mmoja wanarudi mbio mbio, “vipi nyie, mbona mnakimbia?” aliuliza Idd Kibabu, kwa mshangao, “ametushambulia, kumbe bado anayo ile bastora ya jana” aliongea Charles huku akihema hovyo hovyo, “pumbavu mnawezaje kumkimbia kijana mdogo kama huyu, wengine wapo wapi?” aliongea Kibabu na kuwashangaza kidogo wale polisi wa makambako, yani mmoja alie kuwa nae, na mwingine aliekuwa na Charles, maana wao wanacho juwa wana msaka jambazi na sio kijana mdogo, alie zarauliwa na sajenti huyu, “afande inaonyesha yule kijana anauwezo wa kutumia silaha maana ame tumia risasi mbili kwa watu wawili, yani anashabaha kari sana” alisema Charles, hapo Kibabu ni kama aliwaza kidogo, kisha aka watazama wale polisi kutoka makambako, “ok! wewe na wewe, nendeni maka waite wengine mje nao, sisi tunatangulia” alisema Kibabu, kisha wale polisi wakakimbia kuelekea upande kwa kaskazini wakiyafwata makundi ya kati na kushoto, huku njiani wakiulizana maswali tata waliyo kosa majibu yake, “inakuwaje wasema inaonekana anauwezo wakutumia silaha, inamaana huyu jambazi hakuwai kutumia silaha mwanzo?” aliuliza mmoja wa polisi wale, wakati anae mwuliza nae alikuwa anajiuliza swali lile lile,
Wakati wale polisi wanaelekea upande huo, huku nako Kibabu, na askari wake watatu wote kutoka songea, wakiwa na bunduki zao mikononi, walitembea kwa tahadhari kuelekea kule waliko sambuliwa na Edgar, ambako sasa kulikuwa kimya kabisa, baada ya mwendo mrefu kidogo, waliwakuta wale polisi, wakiwa wanaangaika kijipatia huduma ya kwanza, kwenye majelaha yao yaliyo kuwa yanavuja damu kwa wingi sana, “inamaana aliwapiga miguuni tu! alafu unasema kuwa anashabaha” aliuliza Kibabu akiendelea kuwatazama wale askari polisi wa makambako, walio onekana kuwa katika maumivu makali, “amesema kuwa akutaka kutuuwa, ametuacha tuje kuwaambia kuwa wao sio majambazi, nakwamba sasa ana SMG” alisema mmoja wapolisi wale, kwa sauti iliyo jaa maumivu makali, Idd alitabasamu kidogo, huku ana iweka bunduki yake begani kwa kuuvaa mkanda wake, “unazani yupo sahihi?” aliuliza Kibabu, huku ana chomoa bastora yake na kuanza kufunga silent barrer, yani kiwambwa sauti, “inawezekana afande, maana ata yule binti tunae sema ame mteka, inaonekana tofauti kabisa na....” akuwai kumalizia kuongea yule askaari constable, maana ilisikika tyuu!, na hapo hapo damu zika anza kuvuja kwenye paji lake la uso, huku yule mwenzie anashangaa, na kabla ajapata jibu kasona bastora ya kibabu ime mtazama yeye, akajuwa zamu yake imefika, akataka kupiga kelele, lakini hakuwai, ika tyuuu! kimya kimya, akadondoka chini huku na yeye damu zikivuja kwenye paji la uso, wakina Charles wakacheka, kidogo, “nilijuwa tu kwa nini uliwatuma wale wengine” alisema mmoja wa waskari wale wa kutoka songea, “unazani mimi mjinga, tena watakapo peleka miili hii mnjini, lazima taharifa ifike songea, na sisi kuonekana kuwa tupo sahihi kumwangamiza huyu bwana mdogo, na hapo ndipo mapombeka ata acha kuuliza maswali yakijinga” alisema Kibabu, huku anafungua kiwamba sauti, kwenye bastora yake na kuifadhi tena bastora yake, wakati huo Charles aka ongea, “tena ukichukulia kuwa ana smg na bstora, nijambazi kamili” wote wakacheka kidogo, “tutamaliza kazi kiulaini kabisa” wakati huo huo, waliwaona askari polisi wengine wakija mbio mbio, “vipi jamani, nasikia askari wangu wame pigwa risasi?” aliuliza koplo Mapombeka John,
“dah! imeniuma sana, yani huyu jambazi ametuondolea watu muhimu sana” alisema Kibabu kwa sauti iliyojaa uzuni nyingi, “kumbe yule kijana ni hari kihasi hiki?” aliuliza koplo John Mapombeka, kwa sauti ilijaa ghazab, huku ana sogea pale ilipolala miili ya wale askari wawili, kwakwkeli ilikuwa vigumu sana kwa Jiohn Mapombeka, na askari wake kujizuwia kuangusha machozi, machoni mwao, wapo walio diriki kutoa kilio cha wazi kabisa, na mwsho wakaamua kuwasiliana na dereva wa gari moja, wakitumia redio call, kuwa asogeze gari, kuja kuwachukuwa wale marehemu, kwakutumia barabara afifu inayotumiwa na magari ya kubeba miti ya mbao, kupeleka kiwandani, huku na wao wakiwabeba wale askari wawili, na kuwasogeza sehemu ambayo wata wapakiza kwenye gari.
dakika chache baadae tayari gari lilisha pakiza miili ya wale askari, na gari likiwa na askari wawili likaondoka kuelekea mjini, huku Mapombeka wenyewe akiungana na na askari wake, kuelekea mjini, akiwa na lengo la kwenda kuonmgeza askari wengine na silaha, maana alipania kumnasa huyu jambazi, yani Edgar, “nitaakikisha na mkamata na kumnyonga kwa mikono yangu” alisema Mapombeka, kwa sauti kavu iliyo jaa hasira na machungu,
wakati huo wakina Kibabu na askari wake ambao sasa walikuwa pamoja, waligawanyika tena, lakini safari hii ni makundi mawili, yote yakiwa yamechanganya askari wa songea na wa hapa makambako, kundi moja la askari kumi, alikabidhiwa askari mmoja anae itwa Khassim, au wengine umwita kessy, ambae alikuwa msaidizi wa koplo Mapombeka, ambae alisonga mbele kwa mguu, kufwatilia waliko elekea wakina Edgar na Monalisa, wakitumia alama za nyayo za miguu, na nyasi zilizo lazwa na miguu ya wawili hao, huku sajent Kibabu akizungukia upande wa barabara ya ndani kilomita tano toka pale walipo upande wa kusini, yani upande wa Njombe, kama walivyo elekezwa na pc Khassim, akiwa na askari wanane, ukiachilia yeye mwenyewe na dereva wake, wakisisitizana kuhusu mawasiliano.******
Saa tano na nusu, ndani ya ukumbi wa mikutano, kwenye jengo la polisi mkoa, SSP Manase Kingarame, alikuwa amesimama mbele ya jopo la wanadhimu wa jeshi la polisi mkoa, walio zunguka meza mbele ya mkuu wa jeshi hilo mkoa wa Ruvuma, akitoa report ya uchunguzi na oparetion ya kumsaka Lukas, “afande ukiachilia askari wetu kufanikisha kuliuwa jambazi hilo lililokuwa lina pambana na polisi wetu, pia askari wetu wame gundua uwepo wa jambazi mwingine, aliekuwa anashirikiana na jambazi Lukas, hivyo wapo mbioni kumnasa ilikuthibitisha hilo” alisema Kingarame, kwa akika ilikuwa report tamu kwa watu waliokuwa mle ndani, wakimsikiliza bwana Kingarame, “jina la huyu kijana anaitwa Edgar Eric Mbogo” aliongezea Kingarame, huku wale wenzie wanaandika bahadhi ya point, alizokuwa anaziongea bwana Kingarame, “nitakuwa na wapareport kila ninapozipata” alimaliza SSP Kingarame,
Hapo RPC akajikooza kidogo, huku anatabasamu, “hiyo itasafisha jeshi letu, kwa hiyo ongea kwa vyombo vya habari, maana wanchi wakisikia, wata zidisha Imani juu yetu, na huyo jambazi mwingine atafutwe haraka sana” alisema RPC, na baada ya hapo, ikafwata uchangiaji wa hoja na ushuri, huku wengine wakishauri, kabla hawaja tawanyika na kila mmoja kuendelea na shughuli zake, *****
Mida hiyo hiyo ndio mida ambayo, Kanal kisona alikuwa anashuka toka kwenye gari nje ya ofisi yake ndani ya kambi kubwa la jeshi la ulinzi, akitokea nyumbni kwa brigedia Fransis Haule, kumpatia taharifa juu ya kilicho tokea huko Makambako, “nisubiri kidogo, unipeleke nyumbani, nawewe ukapumzike” Kisona aliongea hivyo, huku anaingia ofisini kwake, akipokelewa na mtunza nyaraka ambe alikuwa zamu sikuile, “afande shemeji alipiga simu, amesisitiza umpigie” alisema yule mtunza nyaraka, “ok, atakuwa amenimisi huyo” alitania huyu kamanda kijana, ambae aliingia ofisini kwake, nakuanza kuandika vitu flani akipanga kumpigia simu mke wake, pindi akimaliza shughuli zake.
Nusu saa baadae alikuwa amesha maliza kuandika mambo yake, kisha aka mpigia simu mke wake******
Saa sita na nusu, katika msitu huu pembezoni mwa miji wa Makambako na Njombe, sasa wakina Edgar walikuwa wamesha umaliza msitu washamba la miti, nakuingia kwenye msitu wa kawaida, hali ya hewa ilishabadilika ukungu na baridi vilisha ondoka, kamasio kupungua, Monalisa alikuwa amechoka sana, “Eddy nasikia joto, chukuwa koti lako” alisema Monalisa huku anasimama, nakuvuwa lile koti, na kumkabidhi Edgar, “haya bwana wacha nikubebee, najuwa utalikumbuka baadae” alisema Edgar, ambae pia lisimama, huku analipokea jacket lake, Monalisa akacheka kidogo, Edgar lie ibeba ile bunduki aina ya SMG, kwamtindo wa kuilaza kifuani, nasio mgongoni, alifungalile jacket kiunoni.
Nikama wajiona kuwa wapo sehemu salama, ni baada ya kuwa, wametembea umbali mrefu sana, ndani ya msitu, Edgar alimtazama Monalisa kwasekunde kadhaa, nikama kunakitu alikuwa anakiangali kwa mrembo huyu, kiasi cha kumfanya Monalisa astuke kidogo, nakujiuliza “huyu mbona ananitazama sana, au anataka kunikumbushia mambo yake ya zamani?” aliwaza Monalisa, huku nayeye anamtazama Edgar macho yao yakakutana, wote katabasam, nikama Monalisa alihisi kitu kwenye tabasamu la Edgar, “sijuwi ajuwi kuwa mimi nimchumba wa Erasto?” aliwaza Monalisa akihisi kuwa, pengine inaweza kuwa tatizo, endapo Edgar atagundua hilo, itaendelea.......
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA
KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments: