KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI) SEHEMU YA KUMI NA NNE





ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA TATU:“tulikuja kuulizia vyumba hapa” alisema Monalisa, wakati yeye na Edgar wakiwa wamesimama mbele ya mlango wa jengo moja chakavu la guest house, siliso na jinakipindi hicho waliita guest bubu, wana msubiri mhudumu wa vyumba, ambae tayari walisha mgongea mlango, na kuwaammbia kuwa wamsubiri anakuja, “lakini walisema kuna chumba kimoja tu” alisema tena monalisa,endelea ...........
“tutafanyaje?” aliuliza Edgar, nawakati huo huo mlango ukafunguliwa, akatoka mwanamke mmoja alieonyesha kuwa alikuwa ametoka kulala, “hooo! dada umerudi tena, unabahati sasna kipo chumba kile kile, bado akija chukuliwa na mtu” alisema yule mhudumu, na wao wakatazamana, “tuta fanyaje, chumba kipo kimoja” aliuliza Edgar, na Monalisa nikama akumsikia zaidi alitabasamua na kumtazama mhudumu, “he! afadhari tunaomba utupatie” alisema Monalisa kwasauti ya uchangamfu, usingezania kama, ametoka kwenye timbili timbwili, Edgar akaduwaa, kwauitikiaji wa haraka wa Monanalisa, juu ya kupewa chumba kimoja, “ok! nifwateni” alisema dada mhudumu, huku akiongoza kuelekea ndani, akifwatiwa na Monalisa, kisha Edgar, walitembea kwenye korido fupi na kuishia kwenye mlango mmoja ambao ulikuwa wazi, chumba chenyewe hiki hapa, bafu na choo vile kule” alisema yule dada akiwaonyesha mwisho wa korido, “ngoja niwakee maji ya moto”
Naam baada ya kumlipa elfu tano yule dada, alie dai aina haja ya kujiandikisha kwenye kitabu cha wageni, wakina Edgar wakaingia ndani na kufunga mlango, Edgar akiwa amesimama kati kai ya chumba, akimtazama rafiki yake huyu wazamani, akamwona Monalisa akiweka kijifuko cha vitumbua kitandani na viatu akiviweka sakafuni, kisha akakivua kile kibegi chake na kukiweka kitandani, kisha na yeye akapanda kitandazani na kunyoosha miguu yake, nakuacha nyayo zilizo chafuka kwa vumbi, zikiwa zinaning’inia ukingoni mwa kitanda, akiofia vumbi lisichafue mashuka,
“ebu! niambie vizuri, kwanini wale jamaa wanatufukuza nabunduki?” aliuliza Edgar, huku akimtazama Monalisa, ambae alimsimulia Edgar kilakitu, yani toka alipofika pale hotelini na kwenda kupiga simu, Monalisa, alisimulia jinsi alivyo kutana na yule kijana kwa mala ya kwanza, na alipokutanae kwamala ya pili pale kwa muuza vitumbua, nakwenda kumkabidhi ile tape, kisha kushuhudia anapigwa risasi, hadithi ya Monalisa ilimsisimua sana Edgar, ambe sasa alijuwa hatari iliypo mbele yao, “namfahamu huyo mwnajeshi, Kisona, nilikuwa namwona kipindi baba alipokuwa ananipeleka jeshini kucheza mpira” alisema Edgar kwa sauti tulivu yenye kutafakari, kisha akatulia kidogo, akiwa ameinamisha kichwa, kwa sekunde kadhaa, alafu akainua usowake nakumtazama Monalisa, ambae alitawaliwa na sura ya hofu na uoga mkubwa, “tupo vitani, inabidi tujitaidi tutoke hapa Makambako” alisema tena Edgar, akiwa bdo amesimama pale pale, katikati ya chumba kile afifu chahadhi yachini kabisa, “Eddy, tutaondokaje hapa Makambako, siwata tukamata?” aliuliza Monalisa kwasauti ya unyonge iliyo kata tamaha, nakabla ata Edgar ajamjibu, akauliza tena, na atakama tukitoka tutafika songea kabla hawaja tukamata?” kwakweli Monalisa alionyesha wazi kukata tamaha, “niamini Mona, tutatoka Makmbako, na tutatafika songea Salama kabisa” ilikuwa sauti tullivu yakujiamini toka kwa Edgar, hapo Monalisa akatabasamu kidogo.
“Eddy nitazame miguu, kama nimeumia sana” alisema Monalisa, huku akimtazama Edgar alie kuwa bado amesimama, Edgar aka toa bastora ile yenye kiwambwa sauti, kiunoni mwake na kuiweka kitandani, kisha aka vua begi lake toka mgongoni na kufwatia jacket kubwa, alafu aka, chuchumaa mbele ya miguu ya monalisa na kuanza kumkagua, Monalisa kiwa ana mtazama Edgar alimwona akiitembeza mikono yake kwenye miguu yake, iliyo kuwa ndani ya suruali ya jinsi, akiibinya binya, kuanzia kwenye magoti na kuishusha mpaka chini kidogo, hapo Monalisa akahisi raha flani, Monalisa alitamani kupandisha suluali yake, ili Edgar amminye minye vizuri, lakini akujuwa aanzie wapi, akabaki ana tabaasamu huku anamtazama Edgar, akamwona akiendelea kushusha mikono yake mpaka unyayoni, akaifanya vile vile yani kama anaibinya binya, pasipo kujari vumbi lililojaa kwenye miguu hiyo, yani kama alikuwa anaikanda kidogo, Monalisa sasa alisikia tekenyo ulio mletea raha,
“Ujaumia popotea” alisema Edgar, nikweli Monalisa hakuwa ameumia kama walivyo zania, ila inaonyesha kuwa, Monalisa alisikia maumivu, kutokana na kuto kuzowea kutembea peku peku, “mbona miguu inauma sana?” aliuliza Monalisa alieonyesha kutamani kupewa huduma ile, huku muda wote alikuwa anamtazama Edgar, akimwona kama malaika alietumwa kuja kumwokoa, siwe na wasi wasi ukipumzika kidogo itapoa tu” alisema Edgar kwa sauti tulivu yaupole, “asante EDDY,” alisema Monalisa, huku anatabasamu, hapo Edgar akainuka na kumtazama Monalisa, ambae alikuwa bado anatabasamu, na yeye akatabasamu kidogo, na waka kwepesha macho yao, yasitazamane, mana kila mmoja akiwaza lakwake, wakati Monalisa akiwa anawaza juu ya kuwa Edgar alimchukia toka kipindikile alip chapwa kwaajili ya kumwandikia barua, na kumpatia zawadi ya chupi, Edgar alihisi kuwa Monalisa alisha mchukiaga baada ya ku mtongoza kwa barua, kipindi kile, na ndio maana aliamua kuionyesha ile barua kwa mama yake,
Wakiwa katika mawazo hayo, mala mlango uka gongwa, hapo wote wakastuka, wakati Monalisa ana tazama mlangoni, Edgar akaikota haraka bastora yake pale kitandani, na kuionyeshea mlangoni, Monalisakainuka haraka na kusimama nyuma ya Edgar, “maji tayari, waini kabla ayajapoa” ilisikika sauti ya yule dada mhudumu, wa guest hii yenye hadhi ya chini kabisa, “asante dada” alijibu Monalisa, huku anamtazama Edgar, ambae nae alikuwa anageuza shingo, kumtazama Monalisa, aliekuwa karibu yake kabisa, huku bastora ameielekeza mlangoni, nyuso zao zikiwa karibu kabisa, na macho yao yalipo kutana wote wakatabasamu, “we Edgar kwani unajuwa kuitumia hiyo?” aliuliza Monalisa, ambae akuwa anajuwa umaili wa rafiki yake huyu wa zamani, katika matumizi ya silaha za moto, “ndio najuwa” alijibu Edgar, huku anasogea kitandani na kuiweka tena bastra kitandani, wakati huo Monalisa nae aka sogelea kitandani na kichukuwa kibegi chake kidogo cha mgongoni, “Eddy, nisindikize bafuni ukanisubirie nioge” alisema Monalisa ambae alionyesha uoga wa wazi kabisa, huku ana fungua kile kijibegi chake na kutoa kanga, “basi geukia huko, ni vue sruali bwana” alisema Monalisa kwa sauti ya kulalama, ila yenye utani mdogo, Edgar aliekuwa anaweka bastora kitandani, akageuka na kutazama ukutani, “kanini unaogopa kuoga peke yako?” aliuliza Edgar, akiwa ametazama ukutani, “naogopa kuwa mbali nawewe, watanivamia tena” aliongea Monalisa, kwa sauti flani yakudeka, ******
Ikiwa zimepita dakika chache toka wamendoka wale vijana wawili, wakike na wakiume, Rehema akiwa ana maliza kufanya mahesabu na kutaka kufunga duka lake, mala akasikia “we! dada bado ujafunga duka mpaka saa hizi?” Rehema akasuka na kugeuka kutazama mwongeaji, akaona vijana wawili, “ndio na funga kwani mnashida na dawa” aliliuliza Rehema akiwatazama wale vijana, ambao nikama aliwaona pale kwenye tukio la mauwaji ya Lukas, “sisi ni maafisa wa polisi,” alisema mmoja wao huku akitoa kitambulisho, na kuonyesha, tuna ulizia kama ume waona watu wawili wanapita hapa, wakike na wakiume” alisema yule kijana huku anarudisha kitamburisho mfukoni, hapo kengere ya tahadhari ikagonga kichwani kwa Rehema, akahisi kuwa watu hawa awakuwa na nia nje na hawa vijana kama ilivyo kuwa kwa Lukas, “hapana sijawaona, kwani wamefanyanini” alijibu REHEMA, huku akiwa tazama wale vijana, ambao pasipo kujibu kitu walitimua mbio kurudi walipotoka, Rehema alisimama kwa dakika kadhaa, kisha aka funga dirisha la kuuzia duka lake, nakuzima taa yandani, akaelekea ndani kabisa ya nyumba ile. ******
Roho ilimuuma sana kanali Kisona, kwa kumpoteza Lukas, ukiachilia kupotea kwa ushahidi watukio la mauwaji ya NMC, pia ilimuuma sana kwa kushindwa kumsaidia mtu ambae, aliamini kuwa yeye ndie msaada wake, Kisona lijiona kuwa zahifu sana, kwa kifo cha Lukas, ilifikia atua ya kushindwa kula chakula, ata mke wake doctor Elizabeth, aligundua unyonge wa ghafla wa mume wake, “baba Doto fanya kama uchunguzi unaendelea, naipo siku utafanikiwa” yalikuwa maneno ya mama Kulwa, ambae aliongea huku anaweka mkono wake kwenye kichwa cha mume wake, nakumchezea nywele kidogo, “lakini imeniuma sana, yani niliona kwa macho yangu dalili zote za uonevu” aliongea Kisona, kwa sauti tulivu yakinyoge,
Nikweli bwana Kisona alikuwa amekosa amani kwa tahalifa ya Rehema, “sijuwi nianzie wapi kufwatilia swala hili?” alijiuliza bwana kisona, “lazima kuna ubaba ishaji hapa” aliendelea kuwaza Joseph Kisona, akionyesha wazi kutamani kufwatilia swala hili, *****
Edgar alikuwa amesimama nje ya mlango chakavu wa bafu na choo cha nje, cha hii guest bubu, huku sauti za kumwagika maji zikisikika, “alafu Eddy nimenunua vitumbua vitano umeviona pale kitandani?” ilisikika sauti ya Monalisa toka ndani ya bafu, iliyo mfanya Edgar acheke kidogo, maana alikumbuka mbali sana, “unacheka nini, au utakitena kama ulivyo kataa asubuhi?” aliuliza Monalisa nikama alikuwa anamtega Edgar, kuona atajibu nini, “hapana nita kula tena nina njaa kali sana, sijala toka asubuhi” alijibu Edgar, hapo akasikia kicheko kidogo, “ata mimi sijala toka asubuhi, ngoja nivae alafu tukale”
Dakika chache baadae walisha rudi chumbani kwao, ambako waligawana vitumbua nakuanza kula huku wakiongea hili nalile, lakini hawakuweza kuongelea urafiki wao wazamani, maana akuna mmoja wao alie weza kuanzisha maongezi hayo, ******
usiku hule sajent Kibabu, na kundi lake la askari sita na yule dereva wao, wakisaidiwa na polisi wengine kumu na tano wa hapa hapa makambako, walizunguka mji mzima wa makambako, wakiwasaka wakina Monalisa na Edgar, huku wakibandika matangazo ya kuwatafutwa kwa Edgar, lililo ambatana na picha yake, ikieleza kuwa kijana huyu, ni jambazi anatafutwa na polisi.
Alichokipanga kichwani mwake, sajent Kibabu, ni hatari tupu, “hawa washenzi nikiwakamata, ni8takacho wafanya sitoiona pepo, ata nikiungama zambi zangu” aliwaza sajent Idd kibabu, akiwa anatembea kwenye chochoro moja ya mtaa wa Kambanga, akifwatiwa na askari wake wawili, na sasa baada ya basora, walikuwa wameshika sub Machinegun, (SMG)*****
Jua lilikuwa kuwa linapenya madirishani, na kuwaangazia chumbani ambapo Monalisa alikuwa amejilaza pembeni ya Edgar, alie pitiwa na usingizi mzito, Monalisa aka jiuliza kwanini mpaka mida hii wapo ndani ya chumba hiki, awajaondoka kuelekea songea, akajuwa labda kwakuwa Edgar amechoka sana, hivyo kwa hakiri za za usiku wa manane, akaona amwache aendelee kulala,
Monalisa alimtazama Edgar pale alipo lala fofo, akapata wazo la kumchungulia sehemu zake za siri, sijuwi wazo hilo lilikuja kivipi, basi taratibu Monalisa akaijinyayua na kuanza kufungua mkanda wa suruali ya Edgar, lakini kabla aja anza kufungua, ghafla akastuka kuona mlango wa chumba kile, unafunguliwa na wakaingia wale vijana wawili, waliotaka kumbaka kule kwekenye ile hotel, yani wale walio muuwa Lukas, safari hii wakiwa na mapanga mikononi mwao....(wadau mwenye taarifa ya kkuuwa kwa gari aina ya Toyota wish, bei iwe kuanzia million 6, kushuka chini, liwe katika hali nzuri, anijuliishe in box, ikiwezekana nitumie picha ya gari hilo) itaendelea





(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.