Simulizi: Mateso ya maisha yangu.
Nakumbuka mnamo mwaka 2012 mume
wangu kipenzi alifikwa na umauti akiwa kazini kwake, ambapo kazi yake kubwa
ilikuwa ni kupasua mbao.
Siku hiyo nikiwa sina hili wa lile
muda wa kama saa tisa alasiri, niliisikia simu yangu ikiita, niliichukua simu
ili kutazama ni nani aliyekuwa ananipigia kwa wakati huo, ila namba ilikuwa
ngeni katika simu yangu.
………..Nilibonyeza kitufe cha
kupokelea simu
Hallo.... mimi ndiye niliyeanza
kusema
………..Hallo... nilisikia sauti ya
mwaume.
Shemeji, habari yako ilikuwa ni
sauti ya mwanaume yule.
Salama nilijibu,
………..Samahani nani mwenzangu, Ni
mimi shemeji yako Yuzo.
Oooh shem yuzo kwema? nilihoji.
Kwema kiasi ilikuwa ni sauti ya shem
yuzo, moyo wangu ilishtuka,
kunani tena shem yuzo, sikusita
kuhoji kwani shem yuzo nilikuwa namfahamu fika alikuwa ni rafiki mkubwa wa mume
wangu,
Shem aliendelea kuzungumza huku
akiwa amejawa na simanzi nyingi ndani ya sauti yake,
Samahani shem, najua sina budi
kukupa taarifa hizi ijapokuwa ni ngumu kuamini, aliweke pozi kidogo kisha
akaendelea.
Mumeo kwa bahati mbaya wakati
tunafanya kazi zetu hizi za kila siku amedondokewa na gogo hivyo amefariki.
mmmmmh, niliguna huku nikiwa siamini
kile ambacho nimekisikia,
shem imekuwaje, sikusita kuhoji huku
sauti yangu na machozi yangu navyo vikiwa havipo mbali nami.
Ni story ndefu shem wangu ila jambo
muhimu la kufanya kwa sasa ni kuwaambia
wazazi wake pamoja na ndugu na jamaa wa karibu kuhusu msiba huu, mengineyo
tutakuja kuongea kisha akataa simu.
Kiukweli zilikuwa ni taarifa ngumu
sana kwangu kuzipokea kwa mikono miwili kwani nilihisi zinanielemea, nililia
sana na nilifanya kama ambavyo shem yuzo alivyoniagiza.
**********
Kwa kuwa mwili wa mume wangu ulikuwa
umeharibika sana kutokana na ajali aliyokuwa ameipata, hatukuchukua muda mrefu
kufanya maziko.
Namshukuru Mungu wangu, maziko
yalifanyika salama……. Ila
Kiukweli baada ya maziko maisha
yangu yalianza kubadilika na kuwa magumu sana kupita kiasi, ndugu zangu wote
walitenga nami, pamoja na familia yangu kiujumla.
Sikujua ni nini kimesababisha mpaka
ndugu zangu kuwa vile, ila baada ya kufanya uchunguzi ni kwanini ndugu wameamua
kunifanyia vile, nilikuja kugundua kwamba walifanya vile kwani waliamini na
waliaminishana mimi nimemtoa kafala mume wangu kwani kabla ya kupatwa na umati
tulikuwa na migorogoro ya hapa na pale katika maisha yatu,
Japo ukweli ni kwamba mimi sikuhusika
na hayo waliyoyasema hata kidogo, pia
ukweli ni kwamba mimi na Mungu wangu ninayemuamini ndiye anajua ukweli wote.
Ikiwa mchana, ikiwa giza…. Maisha
yangu na famili yangu yalizidi kuwa magumu sana kila jua lilipokuwa linachomoza,
kila kukicha nilionja uchungu wa maisha, kuna wakati nilikuwa natafakari hivi
kwanini Mimi? Kiukweli nisiwe Muongo maisha yalikuwa ni magumu sana kupita
kiasi.
Pia ikumbukwe kwa wakati huo nilikuwa na
watoto watatu, mkubwa alikuwa darasa tano, mtoto wa pili alikuwa darasa la
pili ila huyu wa tatu alikuwa ni mdogo
sana, ndiyo kwanza alikuwa na miezi mitatu pekee.
*********
Kula kwangu pamoja na familia yangu
kulikuwa ni kugumu sana, kuna wakati nilitamani hata kulitumikia vyema kabila
langu la uhehe kwa kujinyonga, ila kadri nikiwataza wanangu mawazo hayo machafu
yalikuwa yakijitenga nami.
Katika siku ambazo huwa huwa
siisahau ni tarehe 8. 10 2016, siku hiyo
nilibahatika kufanya kazi kwa mama mmoja ya kumfulia nguo zake, nilifanya vile
kwani pesa aliyokuwa ananilipa ilinisaidia kuhakikisha mkono wangu na mikono ya
wanagu inakwenda kinywani.
Mara baada ya kupata ujira wangu
kutoka kwa mama yule nilinunua unga nusu kwa ajili ya kupika chakula cha
mchana. Nilipika chakula kile japo kilikuwa ni chakula kidogo. Kwa kuwa msemo
wa wahenga unasema ni heri mzazi abaki njaa ila wanao wale, hivyo niliungana
kwa kiasi fulani na wahenga hao.
Kwa kuhakikisha nakula kidogo ili wanangu wasijisikie vibaya,
Nilikula kidogo wao nikawaacha wanakula kisha mimi nikaelekea nje kwenda
kumuogesha mtoto wangu mdogo wa miezi mitatu.
Wakati nikiwa nje namuogesha mtoto
wangu mdogo, nilisikia watoto wangu wale wawili ndani wakigombana, ugomvi wao
ulitokana na kutoshiba chakula kwa sababu siku hiyo chakula kilikuwa ni kidogo
kama ambavyo nimesema hapo awali. Ni dhairi hawakushiba.
Kutokana na ugomvi wao kuendelea
kuwa mkubwa, nilimuacha mtoto mdogo ndani beseni lilokuwa lina maji na kukimbia ndani
kwenda kuamua ugomvi wa wanangu. Sikumuacha mtoto mdogo makusudi ila nilikuwa
kama nimechanganyikiwa.
ile nafika tu ndani nakuta mtoto
wangu mwingine ameshika kisu amekwisha mchoma mtoto mwingine kwani walikuwa
wanagombania sufuria ambayo niliipikia chakula. Yule aliyemchoma akaanza
kukimbia kuelekea nje, nami nikiwa katika hasira nilianza kumfukuza kuelekea
barabarani ambapo alipokuwa anakimbilia.
Ile anafika barabarani kwa bahati
mbaya naye akagongwa na gari na kufariki pale pale, ikumbukwe wakati huo mtoto
mdogo nilikuwa nimemuacha kwenye peseni naye alifariki kwa kuwa alikunywa maji
niliyokuwa nayatumia kumuogesha.
Kiukweli hapa nilipo mawazo yangu
yamepupazwa, sielewi moja wala mbili nimeipoteza familia yangu yote kwa muda
mfupi, Sielewi ni nini cha kufanya, maisha yamekuwa ni mtihani usiyo na majibu
sahihi kwangu, naomba japo ushauri wako uweze fariji moyo wangu, kwani haya ni
mateso ya maisha.
Mtunzi; Benson Chonya
bensonchonya23@gmail.com
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA
KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
No comments: