Moto hafunikwi shuka



MIMI sihitaji mkeka; kwani nataka kuswali? Miye hata chini naketi, kikubwa ujumbe ukufike bibiye upooo!?  Kuna mwenzenu mmoja kaninukisha shombo, basi hapa najisikia kichefuchefu cha hatari; na kama mjuavyo pa kutapikia sina zaidi ya hapa kilingeni kwangu. Bibiye kanikuta na mambo yangu nikamuona wa maana kumbe ovyooo, mambo yake kama mtoto! Kweretukweretu mpaka kwangu kuniletea mambo yake na mumewe eti anamshangaa mzee siku hizi kawa na hamu ya tunda kama yote. Akipita huku anataka, akikatiza kule kamenya dodo, mara chali kwenye uwanja; mpambano kama wote.
Sasa ajabu shogaangu kichefuchefu eti hapendi, ndiyo kafunga safari kuja kunitaka ushauri. Nikuambie shoga yangu, alipomaliza kunisimulia aliambulia misonyooo kama yooote. We mahabuba wako yuko moto halafu unachukua kishuka chako unataka kuuzima; utakulipukia ukome mwana kukoma.
Kipindi ambacho moto umewaka ndiyo wakati wa kupika mapishi uyajuayo, weka viungo ujuavyo ili bwana akila ajilambe. Tupia udambwidambwi wote kwenye pishi, mikao nayo isiwe ya kizee; pande nne zote zako, si lazima uangalie kaskazini tu hata kusini kuna kuhusu upooo?
Mambo ya kukimbilia kwa waganga kutafuta dawa za mapenzi wakati dawa mnazo hamtaki kuzitumia yamepitwa na wakati. Laazizi wako anapokuwa na njaa ndiyo wakati wako wa kumpikia ale ashibe ili asidangedange kwa wanuka kwapa.
Kinachonishangaza; shoga zangu wengi wakiona mzee kapandisha mzuka wao ndiyo wanaaza; oooh subiri nikate kucha, mara nakuja ilimradi tu kupoteza muda wa mchezo. Matokeo yake wanakuja kutoa huduma wakati mzee njaa imeshapotea hata akila basi tu; ndiyo hapo wanawake wenzangu wanapoambuliaga viporo kibao vya mapishi yao.
Kesho na keshokutwa wanaaza kulalamika tena; oooh mume wangu siku hizi hali vizuri hata akila ananibakishia viporo; sasa kumbe ufanyweje? Chacha na pishi lako la masharti nani anataka mambo hayo ya “subiri nakuja, natoa mwenyewe.” Siku zote shoga yangu pishi humfaa mwenye njaa, aliyeshiba chake kitanda.
Sasa na wewe kama mpishi mkuu mimi shoga yako, Anti Nasra, kiboko ya mashangingi mjini nakupa somo hili likuingie kichwani. Nadhani unanijua huwa sikoseagi; ukinielewa huna haja ya kwenda kwa waganga kuliwa hela yako kumtengeneza bwana; upooo? Halafu kingine shoga yangu kumbuka sisi ni magolikipa wazuri na sifa ya golikipa ni kudaka?
Wewe maadamu mpira umepigwa na fowadi usiulize kapigia wapi, mara ni dakika ya ngapi hiyo si kazi yako, kilichokuweka langoni ni kutimiza jukumu lako. Bingilika hata kama mashuti yatakuwa sita usiruhusu mpira ukupite, sifa yako ni kudaka upooo shogaangu; visingizio vya sijui nimechoka mara subiri kidogo; utatafutiwa sabu; utashangaa hupangwi kwenye mechi.
Basi kwa leo nijianue chini nikiamini kuwa utakuwa umenielewa ipasavyo; wale wenye masikio gundi shauri yao; mapenzi yana wenyewe na wenyewe ni wenye ujuzi wao. Kwa wale niliowakera wajue ndiyo furaha yangu, misonyo yao iwarudie wenyeweee.


(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.