MAMBO YANAYOKWAMISHA "NDOA" NYINGI NA KUACHA VILIO,...YAEPUKE MNO
Ndoa siku hizi zimekua kama fashion yaan watu wanazikimbilia kwa kukurupuka kisa michango ya harusi, kuiga n. k ila ukweli unabaki hakika yafuatayo yanawaponza mno wanandoa wengi nchini:
1: Wahusika kuingia katika ndoa pasipo kuwa na ufahamu juu ya ndoa. Wengi huingia kwa kufuata mazoea tu kwamba, umri fulani ukifika basi huwa ni wakati wa kuoa au kuolewa. Wengine huingia kwenye ndoa ili kujionyesha kwa jamii tu kwa kuwa na sherehe ya harusi ya kifahari. Watu hao utawagundua mapema tu, maana husisitiza sana juu ya sherehe za kifahari maana hawana future na wewe, hata kukopa kwa ajili ya sherehe wako tayari.
2: Kukosa mifano mizuri ya namna ya kuendesha ndoa imara yenye furaha katika jamii, hususani kutoka kwa wazazi wao. Wazazi wenyewe wamekuwa si mfano mzuri juu ya ndoa bora. Wazazi kuwa ndoa zenye migogoro isiyoisha, imekuwa mafundisho mabaya kwa watoto wao. Kama baba hupiga mke wake, ni wazi kuwa mtoto
wake pia ataishi kwa kupiga mkewe maana hivyo ndivyo alivyoaminishwa na wazazi wake.3: Uvivu wa kujifunza kwa wanandoa nayo imekuwa tatizo kubwa juu ya ustawi wa ndoa. Kumbe wanandoa wanatakiwa kusoma vitabu vizungumziavyo juu ya ndoa, hususani Biblia na vitabu vingine vizuri vifundishavyo juu ya ndoa, kuhudhuria semina za ndoa mara kwa mara na makongamano ya wanandoa tofauti tofauti.
4: Utandawazi. Hii nayo ni changamoto kubwa kabisa kwenye ustawi wa ndoa kwa mfano, 50/50 inayopigiwa chapuo na wanasiasa wanawake na wanaharakati na kumbe si hitaji la mwanamke halisi (mwanamke wa kawaida). Watu hawa wanaopigia debe hii mambo ya 50/50 wana interest zao. Na hivyo, wamekuwa wakiwachanganya wanawake walioko kwenye ndoa.
5: Kuingia kwenye ndoa kwa lengo la kwenda kutumikiwa na siyo kutumika. Ni tatizo kubwa mno kuoa au kuolewa ukiwa na mtazamo kuwa huyo mwenzi wako ndiyo anakuwa mtumwa wako.
6: Kumlazimisha mwenzi wako awe kama unavyofikiria huku ukisahau kuwa kila mtu ameumbwa kwa kusudi fulani maalumu.
7: Kukosa roho ya toba na kusameheana. Ni tatizo kubwa kwamba kizazi kimekuwa kikaidi. Kila mmoja hujihesabia haki, na hivyo kukosa mwenye kuomba msamaha kila mgogoro utokeapo.
8: Mila na desturi nazo ni tatizo hasa wanandoa wanapokuwa wametoka katika malezi tofauti au mila tofauti na bila wao kuwa na uelewa kuwa wanatakiwa kuachilia yale waliyojifunza nyuma ili kuweza kuendandana na wenzi wao.
9: Kukosa commitment juu ya kuwa na ndoa imara, ndoa yenye ushuhuda, ndoa inayomtukuza Mungu. Wengi huishi maisha ya unafiki, wakiwa ndani hawana maelewano hata vitanda wameachanisha, lakini wakiwa nje utadhani hawana mgogoro. Bwana Yesu asifiwe nyingi sana!!
10: Kuamini kuwa ndoa ni kuvumilia hata kama hamna maelewano. Jamii imekuwa ikiaminishwa kuwa ndoa ina shida nyingi hivyo, dawa yake ni kuvumilia msitengane hata kama karibu muuwane. Lakini kumbe ndoa ni maelewano siyo kuvumilia kwa unafiki. Kuvumiliana kupo lakini isipewe kipaumbele inapotosha, maelewano yapewe kipaumbele. Tafuteni kuelewana siyo kuvumiliana. Unakuta mama anasema nipo tu kwa ajili ya watoto wangu na kulinda heshima yangu kwa jamii, kwa nini msitafute suluhu!
11: Ushauri mbaya toka kwa marafiki na jamii kwa ujumla. Kwa mfano, mwanaume kushauriwa kuwa haifai kumuomba msamaha mwanamke hata kama amekosea, eti kwa madai kuwa akifanya hivyo mwanamke atamuona dhaifu! Mwanamke kushauriwa kuwa mwanaume akikukosea dawa yake ni kumnyima unyumba.
Lakini naomba nikuambie kuwa, mwanaume halisi huomba msamaha mapema sana mara tu agunduapo amemkosea mkewe, huyo ndiyo mwanaume halisi. Mwanamke kamwe, kamwe hapa duniani usithubutu kutumia unyumba kama fimbo kwa mumeo, kamwe!
Nakutakia kila la kheri iwapo upo katika ndoa au unatarajia kuingia katika ndoa, Mungu akubariki na kukuongoza. Kumbuka ni bora kukosea kujenga nyumba kuliko kukosea kuoa au kuolewa na mtu asiye sahihi UTAJUTIA MNO
Kama umeipenda SHARE na marafiki
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA
KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
No comments: