MBINU ZA KUMFANYA MWANAMKE AKUPENDE KABLA YA KUMTONGOZA

Ushawahi kujikuta katika hali ambayo unashindwa kujua utaanza vipi kuongea na mwanamke? Ni mwanamke mzuri ambaye moyo wako unamtamani lakini akili yako inashindwa kutengeneza mawazo ya jinsi utakavyoanzisha stori na yeye.
Unabakiwa ukimuangalia akikupita mbele yako, ama mbaya zaidi anakuja kuchukuliwa na wanaume wasiokuwa na thamani yeyote kwa maisha yake. Unabakia na majutio na mawazo ya "kama ningeweza kujiamini mbeleni si ningem...." Well, tatizo hilo halijawahi kutokea kwako pekee bali kwa kila mwanaume wakati flani katika maisha yake na hatutaki lijitokeze tena mbeleni.
So chanzo cha wewe kutoweza kumtongoza huyu mwanamke ni kuwa akili yako ilikataa kutoa mazungumzo ambayo ungeweza kuyatumia kwa huyo mwanamke. Well, waonaje kwa mara moja tukubaliane na akili yako na tusitumie maongezi kuapproach mwanamke, na badala yake tutongoze kimya kimya?
Kutongoza kimya kimya ni mbinu rahisi sana, mwanzo ni rahisi kwa kuwa unapata kujua kama mwanamke anakupenda au la. So bila kupoteza wakati, hebu tuchambue mpango mzima.
Zifuatazo ndizo mbinu unazopaswa kuzitumia ili mwanamke akupende;
Kwa kutumia macho
Kila mtu anajua nishati inayotokana na kutumia macho. Macho ni kiungo ambacho wanaume wamebarikiwa nacho na akikitumia vizuri kinageuka kama silaha nzito wakati ambapo unaitumia kwa mwanamke. Ushawahi kujiuliza ni kwa nini wakati mwingine mwanamke anashikwa na aibu/haya wakati unapomwangalia? Ama je ushawahi kumskia mwanamke akisema kuwa usimwangalie machoni mwake? Hii ni kwa sababu macho yanaweza kutumika kuongea maneno ambayo mdomo unaweza kushindwa kuongea.
Wakati utajipata ukimwangalia mwanamke, mwangalie machoni halafu utoe tabasamu. Kumuangalia kunaonyesha unajiamini. Kutabasamu unamwonyesha kuwa wewe ni salama na anaweza kuongea na wewe.
Mfanye akugundue kupitia kutangamana kwako
Njia nzuri ya kusimama ili wanawake waweze kukutambua ni kupitia utangamano wako na wengine. Kujizunguka na wanawake wengi (haswa wale warembo) kutaashiria ya kuwa wewe ni aina ya mwanaume ambaye wanawake wanapenda kuwa naye. Hii itawafanya wanawake wengine katika hio sehemu kuwa na shauku ya kutaka kujua ni kitu gani ambacho kinakufanya wanawake wapende kuwa na wewe. Hii automatically itawafanya wanawake kuwa na umbea kukuhusu, kuvutiwa kwako, na hata kuingiwa na wivu wa kwa nini haujawaingiza katika kundi lako.
Mbinu hii ni moja wapo ya kiutekaji ya wanawake, kimaumbile wanawake hupenda vitu ambavyo wanawake wengine hupenda. Hivyo kama wewe unamtaka mwanamke flani na hutaki kutumia maongezi, anza kutangamana na marafiki wake wote isipokuwa yeye, mwishowe utamwona akijileta yeye mwenyewe, tena ujitayarishe na mapema kwa kuwa atakuja na presha ambayo kama hukujipanga vizuri inaweza ikakulemea.
Mvutie na mwonekano wako 
Ukitaka kumvutia mwanamke kiurahisi basi ni muhimu kubadilisha mwonekano wako. Mbinu hii tuliieleza kwa kina katika chapisho la jinsi ya kubadilisha mwonekano wako uwavutie wanawake. Kwa kawaida, wanawake wanapenda kushufu wanaume ambao wanavalia kinadhifu.
Lakini hapa usichukulie makosa. Kubadilisha mwonekano hakumaanishi ya kuwa unapaswa kuvalia nguo ghali ama za thamani ya juu. La hasha. Kubadilisha mwonekano kunamaanisha kuvalia nguo safi, nadhifu na ambazo zinaashiria hulka yako. Usijitese kuvalia nguo ambazo haziwiani na wewe kwani kwa mwanamke ni rahisi kukugundua kama umejeuka mwigo.
Wafanye wanawake wakufukuzie 
Kufanya wanawake wakufukuzie inaweza kuwa rahisi sana. Kile ambacho unahitajika ni kutoka nje umakinike na kujifurahisha muda wote. Weka tabasamu katika uso wako na ujiinjoy wewe mwenyewe. Hii itamfanya mwanamke kukunotice na kutamani kuungana na wewe ili muinjoy pamoja.


(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.