VITU HIVI VIMECHANGIA SANA KUVUNJA MAHUSIANO/NDOA NYINGI



1.KUWA MTU WA KULALAMIKA LALAMIKA SANA
Watu wa namna hii huelekeza lawama sana kwa mwenza wake zinazotokana na vitu vidogo vidogo visivyokuwa hata na mikia,miguu wala kichwa,,,kila kinachotokea yeye macho kwa mwenzake tu,,,bakuli tu likidondoka,lawama zinakuwa nyingi utadhani kauwa mtu,,asipompa zawadi kwenye shughuli au vocha na kuchelewa kufika sehemu walipopanga wakutane,,ni full kulalamika hatari hadi unajuta kumfahamu,,kuweni makini,,utampoteza anayekufaa kwa upumbavu wako.
2.UKALI ULIOKITHIRI
Mwenzako tu chumvi bahati mbaya kwenye mboga basi utamkaripikia kama mtoto NA kumuona kama mjinga hajielewi,,akichelewa home tu kidogo hakuna kuuliza kwa staha,wewe ni ukali tu,,amekutania tu basi wewe huchukulii kama utani ni kukaripia tu,,UKWELI NI KWAMBA lugha ya ukali kwa mwenza wako inamfanya moyo wake wa penzi kwako kushikwa na ubaridi,,ataanza kukuogopa na kuanza kutafuta njia za kuanza kuondoka kwako,,usishangae kuona amekuacha hata kama ulimpenda sana,,tumia akili NA hekima kuishi na mwenzako,,huyo siyo mtoto kana kwamba hajitambui.
3.KUISHI MAISHA YA KUIGIZA
Hii hali huwa inafika kikomo na kikomo chake huwa ni kibaya,,ukifeki maisha mwenzako atajua ndivyo ulivyo na wewe ndo unaujua ukweli ndani yako,,unaazima gari ukitaka kwenda kuonana na mpenzi,,akikuuliza la nani unasema lako,,unaazima pamba na anakuona upo smart hatari,,siku anaomba akapaone kwako unampiga sound nyingi,mwisho unaomba uazime gheto kwa mshikaji ili tu kumfurahisha,,,, mjinga sana wewe unategemea siku akija kufahamu yote uliyokuwa unayafanya ni maigizo,,,,,unadhani ataendelea kuwepo na mtu ambae hayupo kiuhalisia na maisha yake ni lazima atatafuta mbadala wa kuondoka kwako,,,labda iwepo NEEMA YA MUNGU, itakayomfanya akuvumilie na kuchukulia hamna namna,,,,,,JIKUBALI WEWE KAMA WEWE KAMA ATAKUPENDA AKUPENDE HIVYO HIVYO ALIVYOKUKUTA NA HALI YAKO.


(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.