ULIMWENGU WA MWANAMKE




Saiko-biolojia ya mwanaume NA mwanamke ina tofauti kubwa sana,,na mwanaume anayeshindwa kujua haya mambo machache kuhusu wanawake,,,ni vigumu kuridhisha au kufurahia moyo wa mwanamke,,,mume nawe mwanaume tambua "ulimwengu wa mwanamke"
MAMBO YAFUATAYO NI MUHIMU SANA MWANAUME KUYATAMBUA;
1.Mwanamke anapenda sana umjali na kumthamini hasa katika mambo madogo madogo ,,,,inaweza kuwa kumnunulia zawadi za kawaida tu mfano lotion,perfume na mengineyo
2.Mwanamke anapenda kusifiwa,,,,msifie mke wako namna alivyotengeneza nywele zake,,viatu alivyovaa na hata namna alivyomechisha na nguo,,,,kwa mwanaume unaweza ona ni jambo dogo bali lina nguvu sana kwa mke anaposikia mume wake amemwambia umependeza
3.Mwanamke anapenda mara kwa mara mwanaume wake amwambie anampenda na hasa umwambie huku unamwangalia usoni au ukitaka njia ambayo ni ya kimahaba sana ,,,,unapiga goti mbele yake na kumwambia"nakupenda sana mke au mpenzi wangu"
4.Mwanamke anapenda mwanaume anayejiamini na yupo tayari kumtambulisha mke wake KWA madaha mbele ya rafiki au ndugu zake
5.Mwanamke anapenda mwanaume anayejivunia kuhusu mke wake sehemu yoyote ile
6.Mwanamke anapenda mwanaume anayekumbuka mambo muhimu kuhusu yeye mfano mume kakumbuka siku ya birthday ya mke wake,siku yao ya ndoa au sikukuu za wanawake.
7.Mwanamke anapenda mwanaume anaye simamia misimamo yake na kutimiza ahadi zake
8.Wanawake wanapenda wanaume ambao wakiwambia nakupenda basi pia waendane na maneno yao kwa vitendo vyao vya kila siku,,namna unavyokuwa tayari kumsikiliza,,kumuheshimu,,kumshirikisha,,,kumsaidia mambo mbalimbali.
9.Wanawake wanapenda mwanaume anaye tambua mchango wa mke wake mfano amesafisha nyumba au chumba chenu vizuri au amefanya shughuli yoyote nzuri,,tambua mchango wake na mshukuru,,kufanya hivyo ni faraja kubwa sana kwa mke wako.

(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.