SIMULIZI: Sitaisahau Tanga (sehemu ya 07)




Nikawaza pale ndani huku nikingoja huko kuoga kwa hisia.
Mara akanipigia simu,
BINTI: Mpenzi upo tayari kuoga?
MIMI: Ndio mpenzi nipo tayari.
BINTI: Haya vua nguo zako zote.
Akakata simu, hofu kubwa ikanitanda moyoni nikawaza kama nivue kweli nguo au la, nikiwa bado naendelea kuwaza akanitumia sms "vua basi ukaoge mpenzi"
Bado nikawa nawaza tu, akanipigia simu
BINTI: Kwani unaogopa nini mpenzi?
MIMI: Hapana siogopi kitu ila naomba kesho ndio nioge kwa hisia mpenzi.
BINTI: (Akacheka sana), kwanini umeghairi mpenzi?
MIMI: Hapana mpenzi ila sijajisikia kuoga usiku huu.
BINTI: Haya usijari mpenzi.
Akakata simu, nikawa nimekaa huku nikipanga mipango ya kesho tu kwenye kichwa changu.
Nikiwa ndani ya mawazo rafiki yangu akinipigia tena simu,
RAFIKI: Kesho nitakuja kukufata hapo kaka twende ile sehemu.
MIMI: Poa kaka.
Alipokata tu simu nyingine ikaingia
BINTI: Mwambie huyo rafiki yako aache kabisa kujihusisha na mambo haya atapotea.
MIMI: Mbona sikuelewi?
Akakata simu, nikazidi kupagawa kwa mawazo hata nisijue cha kufanya kwa wakati huo. Mara taa ya chumbani kwangu ikazimwa kukawa na giza na utulivu uliopitiliza, nikaanza kuogopa huku nikitamani kupiga kelele lakini nikashindwa kufanya hivyo nilikiona chumba kikiwa kikubwa sana, jasho la uwoga likaanza kunitoka nililowa mwili mzima kama nimemwagiwa maji. Mara taa ikawashwa tena na simu ikaanza kuita,
BINTI: Kumbe wewe ni muoga sana eeh!
MIMI: Aaah mmh kiasi tu sio sana.
BINTI: Kukuzimia taa tu jasho limekutoka kama unakimbizwa, nikikufanyia mengine je?
MIMI: hapana usinifanyie vibaya mpenzi.
Akakata simu na kupiga tena,
BINTI: Ooh mpenzi nimesahau, je utapenda tukatembee leo?
MIMI: Aah hapana mpenzi, tutaenda siku nyingine.
BINTI: Kwanini jamani mpenzi?
MIMI: Hamna sababu mpenzi ila tutaenda siku nyingine. Naomba kesho uniamshe mpenzi.
BINTI: Sawa usijari, umekuwa muelewa sasa mpenzi nimefurahi. Ila nakuomba tukatembee.
Akakata simu ilinibidi niwe mpole na nijifanye kuwa nafurahia vyote anavyonifanyia huku akili yangu kichwani ikiwaza mambo mbali mbali ikiwemo namna ya kumuepuka binti huyo.
Nilikuwa nikijigeuza geuza tu pale kitandani huku mawazo mengi yakinitawala.
Mara simu yangu ikaita,
BINTI: Mpenzi leo hulali?
MIMI: Nitalala tu mpenzi si utanishushia neti?
BINTI: Dah nafurahi umenikubali mpenzi, nitakushushia usijari.
Akakata simu, nami nikajilaza pale kitandani. Nikaota ndoto kuwa nipo sehemu nzuri sana na yule binti.

Asubuhi kulipokucha, yeye akawa wa kwanza kunipigia simu. Nikaamka na kwenda kuoga nikarudi na kujiandaa ili nitoke, mara dada akaanza kunipigia,
DADA: Mdogo wangu tafadhari tunahitaji pesa kidogo kwaajili ya kuongezea kulipia hospital na vitu vingine.
MIMI: Hakuna shida dada, kwani mnataka kiasi gani?
DADA: Ungetuma kama elfu thelathini hivi.
MIMI: Sawa natuma sasa hivi kwa njia ya simu.

Nikakata simu na kuanza kutuma pesa, nikafata muamala mzima ila badae naletewa sms kuwa salio halitoshi kuhamisha kiasi cha pesa ninachotaka.
Nikaamua kuangalia salio duh nikakuta eti imebaki mia tano. Nikajisemea 'hata sikubali hawa wendawazimu washaniibia hela yangu kwenye simu yani laki mbili na nusu imebaki mia tano sikubali lazima niwafatie huko makao makuu'
nilikuwa naongea kwa jazba huku nikiangalia lile salio mara mbili mbili bila hata ya kuamini kama hela yangu imekatwa na mtandao kama kawaida ya wizi wao au ni vipi.

Nikaanza kutoka ndani nikiwa na jazba za mtandao ule, mara akanipigia simu
BINTI: Mbona una hasira sana mpenzi?
MIMI: Si hawa wapumbavu wa mtandao wameniibia pesa yangu.
BINTI: Hawajakuibia bhana.
MIMI: Kama hawajaniibia pesa yangu yote imekwenda wapi?
BINTI: Ngoja nitakwambia.
Akakata simu, nikiwa bado nimesimama pale mlangoni huku nina uchungu na hasira ya pesa yangu, mara akanitumia sms
"mpenzi, ulivyoshinda ndani jana na juzi ulifikiri unahudumiwa kwa pesa ya nani? Na tulipoenda kutembea usiku je? Pesa yako imetumika kwenye kukuhudumia kwahiyo usilaumu mtandao, hiyo pesa umeitumia mwenyewe"
ITAENDELEA

(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.