SIMULIZI: Sitaisahu Tanga ( sehemu ya 05)
Nikabaki nimeduwaa tu na macho yamenitoka hata nisijue cha
kufanya kwa wakati ule. Nikaamua kuinuka pale kitandani na kujinyoosha nyoosha
ila cha kunishangaza sikuwa na njaa kabisa.
Nikawa nimesimama huku nikitafakari yale majanga, mara simu
yangu ikaita,
RAFIKI: Vipi wewe mbona umenikatia simu bhana?
MIMI: Hapana sijakata, imejikata yenyewe.
RAFIKI: Halafu wewe naona akili yako imepinda. Haya vipi
itakuwaje, nikupitie kesho asubuhi?
MIMI: (nikiwa bado sijiamini amini kama siku imeisha kweli),
aaah eeh haya poa basi.
RAFIKI: Mbona hueleweki unajiumauma tu, au hutaki? Niambie
bhana.
MIMI: Hapana sio kama sitaki.
RAFIKI: Ila nini sasa? Ongea bhana mtoto wa kiume acha
kujiumauma hapo.
MIMI: Aah sijui bhana
Nikajikuta nimekata ile simu, hata nilikuwa sijielewi
kabisa. Mara dada akawa anapiga
DADA: Yani mdogo wangu siku hizi kweli umekuwa shetani, toka
asubuhi hadi muda huu unashindwa hata kutujulia hali? Yaonyesha umefurahishwa
sana na yaliyo mpata mwenzio.
MIMI: Samahani dada, naomba mnisamehe sana sio kusudio
langu.
DADA: Ila ni kusudio la nani?
MIMI: Sijui dada.
DADA: Hivi wewe una kichaa au?
Nikakata simu kwani naona wananichanganya tu na wakati
sijielewi kabisa.
Nikakaa chini na kujiinamia huku nikipanga mipango kuwa
niondoke mahali hapo hata nikalale nje ili nisipitilize tena. Mara simu ikaita,
BINTI: Mambo mpenzi, nimekumiss.
MIMI: (hapo natamani hata kumtukana), poa tu hata nami
nimekumiss pia.
BINTI: Unaonaje leo twende tukatembee mpenzi?
MIMI: (huku nimejawa na hasira), unajua usinichanganye wewe!
Tukatembee vipi wakati tuko mbali mbali?
BINTI: Ndio unanikaripia eeh!
MIMI: (Nikawa mpole tena), hapana mpenzi nisamehe.
BINTI: Sijazoea kukaripiwa, umeniudhi sana.
Akakata simu, dah nikapagawa zaidi. Nikainuka tena na kwenda
hadi mlangoni ili nifungue mlango nitoke. Mara simu ikaita,
BINTI: Unaenda wapi?
MIMI: Aaaah eeeh mmh!
BINTI: Unakwenda wapi?
MIMI: Aah maswali gani tena hayo?
BINTI: Wewe kiburi eeh!
MIMI: (nikiwa na hasira na mimi), niache bhana nikapunge
upepo nje.
BINTI: Kumbe wewe ni kiburi na jeuri!!
MIMI: Ndio mambo gani hayo jamani mpenzi?
Akakata simu, nikiwa bado nimesimama pale mlangoni
akanitumia sms
"huendi popote"
Nikajikuta nikiwaza mambo mengi, mara dada akaanza kupiga
tena.
DADA: Vipi na leo unakuja au huji?
MIMI: Aaah daah sijui bhana.
DADA: Hivi mdogo wangu una nini wewe?
MIMI: Sielewi kitu dada.
DADA: Uko wapi sasa hivi?
Ile nataka kumjibu simu ikakatika, kuichek eti imeisha chaji
nikaamua kwenda kuichomeka kwenye chaji, huku mawazo mengi kichwani yakiwa
yamenitawala. Nilipokaa kidogo nikaiwasha tena na hapo nikakutana na sms kutoka
kwa binti wa kitanga,
"nimekwambia leo huendi popote, utakula jeuri
yako"
ITAENDELEA
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA
KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
No comments: