SIMULIZI; Sitaisahau tanga (sehemu ya 12)



Nikashindwa kujielewa kwa wakati huo niamue jambo gani, yule mdogo mtu akawa amenikazia macho huku yakiashiria kuwa anangoja jibu langu. Sikujielewa kabisa na wala sikuelewa niwaambie kitu gani. Yule mdada akaniambia kuwa niamue moja. Nikajikuta macho yakinitoka nilitia huruma sana na nilisononeka mno, mara yule aliyekwenda kuleta moto akarudi na ubani ukawashwa.

Yule mdogo mtu bado akaniashiria kuwa nichague ndugu yangu mmoja kwa kafara,

MIMI: Tafadhari nawaomba, ndugu zangu wasitendwe vibaya. Mimi ndio chanzo cha haya yote, naomba sana kama itawezekana basi hiyo kafara nitolewe mimi.
Nilijikuta nikiropoka kwani nilipatwa na mfadhaiko mkubwa yani atolewe ndugu yangu kafara kwa makosa yangu! Hapana huruma ilinijaa.

Yule dada akanikazia macho tena, mara akaanza kuungurumisha kama simba nikawa naogopa huku jasho jingi likinitoka, mara yule mdada akaanza kuongea na mimi tena kwa sauti ya mtetemesho.

MDADA: Kwahiyo upo tayari kafara utolewe wewe mwenyewe?
MIMI: Ndio nipo tayari.
MDADA: Nipe sababu kubwa iliyokufanya kuamua hivyo.
MIMI: Sababu mimi ndio chanzo cha yote haya, ndugu zangu hawahusiki.
MDADA: Upo tayari kweli?
MIMI: (Huku nikitetemeka), ndio nipo tayari.
MDADA: Kweli kabisa kabisa upo tayari!
MIMI: (Nikizidi kutetemeke, huku nikitamka kwa sauti ya chini), ndio.
MDADA: Ngoja nikuonyeshe kwanza.
Nikiwa nimekaa chini huku natetemeka, nikamuona yule dada akichukua kama unga unga kwenye mkoba wake na kunipulizia, nikajikuta nikianguka chini.
Niliposhtuka ilikuwa ni mahali pengine kabisa, kwanza kabisa ilikuwa kama porini tena kumetulia kabisa ni sauti za ndege tu zilizosikika, nikainuka mahali hapo na kuanza kutembea bila ya kujua ninapoelekea, mara akatokea mtu mbele yangu na kunishika mkono huku akinipeleka ninapotakiwa kwenda.
Tukafika mahali kuna nyumba ila ukiziangalia ni kama vichuguu, nikaingizwa chumba cha kwanza humo nilikuta maji yakitokota kwenye pipa kubwa na yule aliyenipeleka akaniamuru nidumbukie kwenye lile pipa ila nikasita huku nikiomba msamaha, ila wala haikusaidia nilimshuhudia yule mtu akinibebea juu juu na kunitumbukiza kwenye hilo pipa linalochemka maji kwakweli nilijua hapo ndio nakufa jamani, ama aliyesema kufa hufi ila chamoto utakiona wala hakukosea. Niliungua sana mule pipani, mara kuna mtu akaja kuniopoa kumwangalia ni yule yule mtoto wa kitanga, akawa anacheka sana.
BINTI: Vipi umejisikiaje hapo?
Nikataka kumjibu ila nashangaa sikuweza kufanya hivyo kwani mdomo ulikuwa mzito sana, akaniambia tena,
BINTI: Nina uhakika kama ukipona na haya nikufanyiayo hutorudia tena kubeba mizigo ovyo ovyo. (akacheka sana na kutoweka).

Nikawa natetemeka mahali pale ila kilichonishangaza ni kuwa nimechemka kwenye lile pipa halafu sijababuka mwili, mara akaja yule mtu aliyeniongoza mwanzo na kunishika tena mkono kunipeleka sehemu nyingine.

Tukaingia chumba ambacho akaniacha mimi peke yangu na yeye akatoka, yani chumba kilikuwa na siafu wengi sana walining'ata kila sehemu ya mwili wangu hadi nikajihisi mwili unakufa ganzi kwakweli ni maumivu yaliyopitiliza.
Baada ya muda akaja na kunifungulia nikatoka mule ndani nikiwa na madonda ya kila aina. Akaniuliza,
"unapenda sana wasichana?"
Nikatikisa kichwa nikiashiria hapana. Akanichukua na kunipeleka sehemu nyingine.

Tulifika sehemu ambayo mbele yake kuna wasichana wazuri sana tena wa kuvutia, yule mtu akanigeukia na kuniambia,
"kijana chagua mmoja hapo"
Nikakataa kwa kichwa kuwa simtaki yeyote, sikuwa na hamu na msichana yeyote kwakweli, yule mtu akaniambia tena,

"inamaana huwaoni walivyo warembo wale mabinti?"
Nikatingisha tena kichwa kuonyesha kwamba siwataki wale wasichana.
Tukaondoka mahali hapo, nikapelekwa sehemu ambayo nilikuta wanaume wenzangu wamepanga foleni halafu kuna mtu mmoja mbele ana panga kubwa sana yani ukimkaribia anakuchinja kama kuku dah nilihisi kupagawa nikatamani kukimbia ila sikuweza, yani yule mtu hakuwa na huruma kabisa kila aliyemfikia alimchinja kama kuku na mimi nikawekwa kwenye huo mstari.
Niliona mwisho wangu umekaribia, nikamaliza sala zote kimoyomoyo nikajikuta nikitubu kila aina ya dhambi niliyotenda, machozi yalinibubujika kila hatua niliyomsogelea yule mtu, nilijikuta nikilia kama mtoto mdogo sikuwa na jinsi zaidi ya kujisogeza ili nikabidhi kichwa changu iwe halali yao.

ITAENDELEA

(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.