SIMULIZI: Sitaisahau Tanga (sehemu ya 08)



Nikakosa raha kwakweli, nikachukia moyoni na kuwaza mwisho wa mambo haya ni lini. Mara dada akanipigia,

DADA: Vipi tena mbona hutumi hiyo pesa?
MIMI: Aaah mmmh kuna tatizo kidogo dada ngoja nitatuma badae.
DADA: Nilijua tu mxyuuuu(akanisonya).
Akakata simu, bado akili yangu haikuwa sawa hadi pale mlango wangu ulipogongwa, nikaenda kufungua kumbe ni rafiki yangu alikuja kama alivyoniahidi jana.
RAFIKI: Vipi upo tayari tuondoke?
MIMI: Ndio nilikuwa nataka kutoka hapa kaka.
RAFIKI: Basi twende.
Mara simu yangu ikaita, nami nikaipokea,
BINTI: Mwambie rafiki yako aache kufatilia mambo yangu.
MIMI: Kivipi jamani mpenzi?
BINTI: Inamaana hujui rafiki yako amefata nini?
MIMI: Hapana sijui.
BINTI: Hivi unajua kama ninaouwezo wa kuwazuia msitoke hapo?
MIMI: Kwani vipi mpenzi mbona sikuelewi?
BINTI: Mpe rafiki yako simu nimuulize kitu.

Nikampa rafiki yangu simu ili aongee na yule binti, kilikuwa ni kitendo cha kufumba na kufumbua yani baada ya kumkabidhi simu rafiki yangu ili aongee naye nikashtukia rafiki yangu akianguka chini na povu jingi likimtoka mdomoni, moyo ukanipasuka kwakweli nilijikuta nikitetemeka na kuona baridi ila jasho jingi likinitoka. Kwakweli nilichanganyiki
wa nilitamani ardhi ipasuke nidumbukie.

Nilimwangalia rafiki yangu pale chini akiwa katulia tuli hata nisijue cha kufanya, nikatamani kupiga yowe la msaada. Nilipotaka kufanya hivyo, simu yangu ikaita
BINTI: Usithubutu kupiga kelele kama unapenda kumuona rafiki yako akiendelea kupumua.
MIMI: Nihurumie tafadhari nakuomba nihurumie.
BINTI: (Akacheka sana).
Akakata simu, mapigo ya moyo yalikuwa yananienda kwa kasi balaa.
Sikujua msaada gani nimpe rafiki yangu pale chini. Nikainama na kujaribu kumuinua ili nimuweke kitandani ila alikuwa mzito kama jiwe tena alizidi kukoroma na povu jingi likimtoka mdomoni. Hofu ikazidi kutanda moyoni mwangu na mawazo mengi yakinitawala huku nikiomba sala zote ili nikomboke na lile janga.

Nikakaa pale chini karibu na rafiki yangu, nikatamani nichukue simu na kuwapigia watu ili niombe msaada ila nikasita kufanya hivyo.
Nikajifikiria tena, ikabidi nichukue simu nimpigie kaka.

MIMI: Hallow kaka nina matatizo tafadhari njoo nyumbani kwangu.
KAKA: Kwani vipi tena mdogo wangu?
MIMI: Tafadhari kaka njoo.
KAKA: Poa nakuja mdogo wangu.
Nikawa na matumaini ya kupata msaada sasa.
Mara kidogo yule binti akanipigia
BINTI: Aliyekutuma umpigie kaka yako simu nani?
MIMI: Aaah eeh sijui hata sielewi.
BINTI: Unampenda kaka yako?
MIMI: Ndio nampenda.
BINTI: Kama unampenda mpigie tena simu sasa mwambie asije.
MIMI: Itakuwaje sasa?
BINTI: Fanya kama nilivyokwambia.
Akakata simu, hata sikujielewa kwakweli nikachukua simu na kumpigia tena kaka lakini namba yake ikawa inaita tu bila ya kupokelewa.
Baada ya muda kupita kupita, kaka akanipigia simu.
KAKA: Nakaribia kufika mdogo wangu, naona missed call yako hapa vipi ulikuwa unasemaje?
MIMI: Nilikuwa nakwambia basi tena usije.
KAKA: Hebu acha ujinga wako huo, nimetoka haraka haraka nyumbani halafu unasema nisije tena! Mi nakuja.
MIMI: Dah usije kaka, tafadhari usije.
KAKA: Kwani kuna nini wewe? Nakuja bhana.
Akakata simu, nikawa ni mtu mwenye mawazo hata nisijue cha kufanya tena muda ule huku nikihofia maisha ya kaka yangu.
Nikamwangalia tena rafiki yangu pale chini, nikamfikiria na kaka yangu anaekuja nguvu ziliniisha kabisa. Mara akanipigia simu,
BINTI: Umeshindwa kabisa kumzuia kaka yako kuja hapo?
MIMI: Nimeshindwa, nihurumie tafadhari.
BINTI: Nitakachokifanya usinilaumu badae.
MIMI: Jamani nihurumie, nihurumie nakuomba.
BINTI: Huruma yangu utaiona akifika kaka yako mahali hapo.
Akakata simu, nikawa kama mtu aliyepagawa. Nikachukua simu na kumpigia dada,
MIMI: Tafadhari dada nakuomba umzuie kaka asije kwangu.
DADA: Kwani kuna nini?
MIMI: Hamna kitu ila mzuie.
DADA: Una matatizo gani wewe?? Na mimi nakuja huko nijue kinachoendelea.
MIMI: Mungu wangu, dada nakuomba usije.
DADA: Khaaa, nakuja sasa.
Akakata simu, nikazidi kuchanganyikiwa nilitamani hata nipae nitokana na haya maswahibu.
Yule binti akanitumia sms,
"ndugu zako wanacheza na moto"
ITAENDELEA

(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.