SIMULIZI: Sitaisahau Tanga (sehemu ya 04)
Nikakosa raha kabisa, nikarudi na kukaa kitandani nikaamua
kujilaza nikitafakari, mara sms ikaingia kwenye simu yangu kuangalia ni yule
binti wa kitanga "angalia mezani nimekuletea chakula"
Loh nikainuka kama nimepigwa shoti vile, kuangalia naona
juisi ya Azam mango na biskuti, nikawaza kuwa ameletaje vitu vile nikaanza
kupata mashaka, mara sms nyingine ikaingia
"usiogope mpenzi, kula tu"
Nilikosa amani kwakweli, nikasogelea ile juisi na kuiangalia
kama ni juisi kweli ndio ilikuwa Azam mango kabisa na ndio juisi niipendayo,
mmh nikaziangalia na zile biskuti zilikuwa biskuti za ukweli kabisa zile zenye
mchanganyiko wa chokleti, kutokana na njaa yangu nikaanza kuvifakamia huku bado
niliwaza ameletajeletaje.
Nilipomaliza tu, akapiga simu.
BINTI: Vipi mpenzi umeshiba?
MIMI: Ndio nimeshiba, kwani umeviletaje?
BINTI: Hata kushukuru hujui?
MIMI: Samahani mpenzi nilijisahau.
Akakata simu, nikakaa na mawazo pale kitandani. Mara simu
ikaita kuangalia ni dada anapiga tena.
DADA: Vipi wewe yani huna hata hofu na mwenzio?
MIMI: Aaah dada samahani.
DADA: Kwahiyo unakuja au huji?
MIMI: Aaah sijui dada.
DADA: Hujui nini? Nipe jibu moja, unakuja au huji?
MIMI: Sitaweza kuja kwa leo dada, nitakuja kesho.
DADA: Nilijua tu, mxyuuuu (akanisonya na kukata simu).
Nikawa pale kitandani nimejiinamia tu huku kichwani mawazo
mengi yamenitawala, mara sms ikaingia kwenye simu yangu
"si ulale mpenzi wangu jamani"
Nikaamua kujilaza huku nikijiona bonge la boya maana nipo
kama vile mtu anayeongozwa na rimote.
Mara usingizi ukanipitia pale kitandani, nililala hadi
nikajisahau nikaja kushtushwa na mlio wa simu.
RAFIKI: Vipi kaka mbona leo hujatokea maeneo?
MIMI: Kivipi ndugu wakati ndo kumekucha!
RAFIKI: (huku akinicheka), kumekucha wakati saa kumi na moja
jioni hii?
MIMI: (nikafungua pazia na kuchungulia dirishani, kumbe
kijua cha jioni ndio kipo ukingoni), acha masikhara bhana saa mbili hii (huku
nikiangalia saa yangu ya ukutani).
RAFIKI: (Akinicheka tena), wee boya saa kumi na moja hii
labda kama leo una kazi ya ulinzi ndio mida ya kujiandaa hii (akinicheka tena).
MIMI: (Nikiangalia vizuri ile saa ya ukutani, iliyoonyesha
mshale mdogo kwenye tano na mkubwa kwenye nane), daah nilichanganya mida kaka.
Nikakata simu na kuanza kuwaza imekuwaje nimelala hadi
kujisahau vile, ni usingizi wa namna gani ulinipata dah!! Mara rafiki yangu
akaanza kupiga tena.
RAFIKI: Kaka, vipi ule mpango wa kwenda kwa mtaalam au
umepotezea?
MIMI: Hapana sijapotezea kaka, nataka sana unipeleke
itakuwaje sasa?
RAFIKI: Wewe tu, nilitaka nikupeleke leo au unaona yale
majanga yako ya kawaida kaka?
Kabla sijamjibu simu ikakatika, na kuanza kuita tena
kuangalia ni binti wa kitanga.
BINTI: Ulikuwa unaongea na nani?
MIMI: Rafiki tu mpenzi wangu.
BINTI: Ulikuwa unaongea nae kuhusu nini?
MIMI: Hamna kitu ni salamu tu.
BINTI: Unanificha sio?
MIMI: Hapana sijakuficha huo ndio ukweli.
BINTI: Wee ni muongo eeh!! Haya njia ya muongo fupi na mi
naijua.
Akakata simu, nikabaki kwenye maswali na viulizo vya kila
aina. Kwanza nikawaza juu ya usingizi niliolala hadi kusahau kuamka kwenda
popote pia kusahau kula. Nikajiuliza inamaana sijala chochote tangu nilipokula
juisi na biskuti usiku. Mara sms ikaingia,
"usijari mpenzi kula na kuoga na vyote vya muhimu
umefanya ndotoni"
Aaah majanga haya!!
ITAENDELEA
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA
KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments: