SIMULIZI: Sitaisahau Tanga (sehemu ya 03)
Nikawaza sana juu ya upotevu wa pesa yangu, nikajiuliza
inakuwaje mtu ufanye matumizi ya pesa ndotoni? Likanijia wazo kuwa yule binti
si mtu wa kawaida. Nikajishauri kwenda kupata ushauri kwa rafiki yangu wa
karibu. Wakati natoka kwenye chumba changu kuna sms ikaingia kwenye simu yangu
ila nikaipotezea sikuisoma wala nini.
Nikaenda kwenye shughuli zangu, badae nikaenda kwa mshikaji
wangu kumweleza kama nilivyowaza. Nikamkuta na tukapiga story mbili tatu badae
nikamweleza mambo yote.
MIMI: Ndio hivyo bhana.
RAFIKI: Aaah pole sana mshikaji wangu ila nilikwambia kuwa
makini na Tanga, hata hivy usipende kuwatongoza mademu hovyohovyo sehemu yoyote
ile.
MIMI: Sasa nishauri ndugu cha kufanya.
RAFIKI: Cha msingi tumtafute mtaalam twende, haya mambo ya
kishirikina kaka.
MIMI: Dah umenitisha kaka hata kurudi kwangu naogopa.
RAFIKI: Usiogope wangu, wee nenda tu ukiogopa atakushtukia
mapema.
MIMI: Dah sijui kama nitalala leo kaka.
RAFIKI: Usijari kaka, cha msingi potezea kama hujui kitu
vile halafu kesho twende kwa mtaalam kaka.
MIMI: Poa kaka nashukuru maana nishapagawa hapa.
Tukaagana pale halafu nikarudi kwangu.
Nikiwa chumbani nikachukua simu yangu kuikaguakagua nikakuta
missed call kibao na sms moja nikashangaa hata ilikuwaje sikusikia wakati
inaita, kumchek aliyekuwa anapiga ni demu wangu wa Dar na ile sms ni kutoka kwa
binti wa kitanga, iliandikwa "usijaribu kumweleza yoyote juu ya habari
zangu" nikashtuka sana, ni hii sms niliyoipotezea wakati naondoka asubuhi.
Mara simu ikaanza kuita, kuangalia ni dada yangu anapiga
MIMI: Hallow dada,
DADA: Mbona umekuwa na akili fupi sana wewe? Unajua matatizo
aliyoyapata mchumba ako huku?
MIMI: Kwani kafanyeje tena dada?
DADA: Muda wote amekupigia simu hupokei, mwenzio yupo hoi
huku ule ujauzito umetoka.
MIMI: (Hata nilisahau kama demu wangu wa Dar alikuwa na
mimba yangu) nini dada mbona sikuelewi?
DADA: Huwezi kunielewa kwa simu, kama unaweza njoo hospitali
au njoo nyumbani.
MIMI: Poa dada ngoja nijiandae.
Nikakata simu, nikaenda kuoga na kuvaa fastafasta niondoke,
wakati nataka kutoka simu yangu ikaanza kuita, kuitoa na kuiangalia ni yule
binti wa kitanga.
BINTI: Unataka kwenda wapi?
MIMI: Aaah hapana siendi popote.
BINTI: (Akacheka kidogo), unataka kwenda wapi?
MIMI: Eeeh aaah nataka kwenda kutafuta chakula.
BINTI: Haya rudi kakae, chakula nitakuletea leo.
MIMI: (Huku nikiwa na hofu moyoni), utaniletea kivipi?
BINTI: Kwani shida yako ni chakula au ni nini? Kama ni
chakula sasa mashaka ya nini si nimekwambia nitakuletea au?
MIMI: (nikaamua kujigeresha kidogo), aaah Acha utani bhana
mpenzi wangu, unajua wazi upo mbali sasa chakula utakiletaje?
BINTI: Nitakileta kwa hisia na utashiba kabisa kwahiyo
usitoke.
Akakata simu, nikaanza kuwaza itakuwaje sasa na vipi kuhusu
kwenda hospitali nikawaza cha kufanya, au niende halafu akipiga nimwambie
sijaenda? Bado nikawa na utata moyoni. Nikainuka pale nilipokaa na kujipa moyo
kuwa naenda tu hata iweje. Nikaenda mpaka mlangoni ile nataka kufungua mlango
tu sms ikaingia kwenye simu yangu, kuangalia ni demu wa kitanga
"nimekwambia usitoke"
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA
KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments: