PROGRAM YA SIMU YAWAWEKA WAISLAMU CHINA PABAYA







Shirika la Kutetea Haki za Binadamu Human Rights Watch limeeleza wasiwasi wake kuhusu programu ya simu inayotumiwa na serikali ya China kuwafuatilia na baadae kuwakamata raia wake wa Kiislamu nchini humo katika mkoa wa Xinjiang.

 Ripoti hiyo mpya imesema mamlaka za mkoa wa Xinjiang zinafuatilia Waislam kwa kuzingatia jinsi wanavyotangamana na majirani zao, iwapo wanaepuka kutumia milango ya mbele ya nyumba zao, au wanaepuka kutumia simu za mikononi, kama wanatoa michango misikitini, na kama wanatumia kiwango cha kupindukia cha umeme majumbani mwao.

Mtafiti wa shirika la Human Rights Watch,Maya Wang amesema utafiti wao umeonyesha kwamba maafisa wa polisi katika mkoa huo wa China wanakusanya taarifa kuhusu tabia za watu ambazo si kinyume cha sheria lakini wanazitumia dhidi ya watu hao. Sera za China zinazotumika katika mkoa huo wa Xinjiang zimekuwa zikikosolewa kimataifa, kutokana na kwamba zaidi ya watu milioni moja wa jamii ya Uighur na Waislamu wengine katika mkoa huo wanashikiliwa katika kambi maalum.


(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.