MWANAMKE USISIMAMISHE NDOTO ZAKO KWA AJILI YA MWANAUME



Mwanaume si mume wako anakwambia sitaki ufanye kazi fulani?si mume wako anakwambia sitaki usome,,si mume wako Anakwambia usijenge kwanza,,sijui na vingine Vingi na wewe unakubali,,,mbona unakaa kama umezaliwa jana,,mbona unakaa kama hujawahi kuachwa au umekaa kama hujawahi kukutana na mtu aliyeachwa,,,,
Naomba nikuulize hivi huyo mwanaume si alikuwa na x wake?si waliachana ndo akaja kwako?hivi hujiulizi kama na huyo x alishaambiwaga hayo mambo?hujiulizi yeye kaachwa wewe nani usiachike?una kipi cha maana ambacho wengine hawana?sisemi atakuacha lakini usisimamishe ndoto zako kwa ajili ya mwanaume,,
Si lazima mwanaume kukuoa kwa kuwa alikuambia uache kazi,,si lazima kukuoa kwa kuwa alikwambia usiende chuo,,si lazima kukuoa kwa kuwa alikwambia uibebe mimba kwanza,,,kama hajakuoa bado basi jua bado anatafuta mchumba,,anaweza kukuchoka au kukuacha muda wowote na hakuna kilio au laana yoyote itamshika maana hamna kitabu cha dini kinasema mtii mwanaume ambaye si mume wako,,
Kuacha kazi,,kuacha chuo,,kubeba mimba vyote ni viherehere vyako MWENYEWE,,,siku akiona mwanamke mwingine na akavutiwa nae kama alivyoachana na x wake basi ndo atakavyo achana na wewe bila kujali ulikuwa unaenda kufanya kazi ikulu au ulikuwa unaenda kusoma marekani,,bila kujali umembebea mimba au umemzalia mapacha,,akikuchoka kakuchoka maisha lazima yaendelee,,hivyo usifanyee kitu kwa kuwa mchumba wako kasema fanyaa,,fanya vitu kwa kuwa unataka

(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.