MKASA: NAJUTA KUINGIA PENZINI NIKIWA CHUO!!




Naomba msome kwa makini sana haya yaliyonikuta, hasa kwa wadogo zangu ambao bado mpo vyuoni mkiendelea na masomo
yenu.

Miaka mitatu iliyopita nikiwa mwaka wa kwanza pale chuoni kwetu, nilibahatika kukutana na kijana mmoja ambaye tulizoeana na kuwa kama ndugu na na baadae taratibu tukaanza kumezwa na zimwi la mapenzi.
Mapenzi yalizidi mpaka nakumbuka tukaanza kukaa katika chumba kimoja kama mtu na mme wake mtarajiwa.

Tuliishi kwa kupendana ule mwaka wa kwanza na hatukufichana kitu tuliweza kushare kila kitu kuanzia fedha mapaka material ya kusomea.
Nakumbuka mwaka wa kwanza sikuwa nimepata mkopo kutoka bodi ya mikopo ila mwaka wa pili jina likatoka na siku hela zilipoingia, jamaa aliniomba nimpe hela kamamkopo kuna biashara ya kuuza simu, flash disk na laptop pale chuoni.

kwa kuwa tayari tulishapanga kuja kuishi wote mara baada ya kuhitimu mafunzo niliona ni poa tu kwani ilikuwa sawa na kutoa fedha mfuko wa kulia na kutupia mfuko wa kushoto.

Nilimpa keshi 1,000,000/= baada ya kuchanganya na akiba yangu tena sikubaki na hata akiba kwani aliniahidi atapunguza kidogo jumatatu iliyofuatia.
Cha ajabu ni kwamba baada ya kupata zile hela sikumwona tena na simu ikawa haipatikani mpaka wiki moja baadae aliporudi tena nilikutana nae wakati twaingia lecture room akiwa kaongozana na rafiki yangu wa kike almaarufu kama Mwajuma.
Moyo ulinipasuka nikamkimbilia na kutaka kumhag akanikwepa na kuonyesha kama hanijali vile. iliniumiza hasa ukizingatia ilikuwa mbele ya watu na wote walijua mahusiano yetu. Basi jioni baada ya kutoka darasani nilimwendea na kutaka kujua kulikoni, alinifokea sana.

Baada ya siku mbili tatu za kutojua nini kilimsibu na anaishi wapi niliaza pata habari kuwa anaishi na Mwajuma na pia ziku chaze zilizopita walisafiri kwenda Dodoma kula bata. Duh?????? Kweli moyo ulinipasuka ilinibidi nimfuate na kumuuliza vipi kuhusu ile hela.

Alinikana kata kata kuwa sikuwahi kumpa, nilirudi room na kulia usiku kucha, Nikawaza ni jinsi gani alivyonifanya nitoe zile mimba zake na kunitumia kisha ananiacha na kumchukua rafiki yangu na je vipi kuhusu hela zangu?
Niliishia kujuta sana na kuendelea na masomo yangu. tangu kipindi hicho sina kabisa hamu ya kuwa na mahusiano ya aina yoyote ile.
Funzo

Wadogo zangu mliopo vyuoni, ni vyema mkaishia kusoma na kutumia muda mwingi kujijenga kielimu kwani ni asilimia chache sana ya mapenzi ya chuo ambayo huishia na mwisho mzuri.

Wengi mapenzi huishia pale wanapohitimu,na wengine hupata bahati ya kurudi nyumbani wakiwa na mimba na watoto wa baba ambao kamwe hawatakuwa msaada kwa familia hizi.

Lakini pia wengi hupatwa na misukosuko ya ajabu na hata magonjwa.
Ni vyema kutafakari kabla ya kujitupa katika mapenzi ya vyuoni


(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.