MAJI YAMTOA CHOZI MBUNGE WA ULYANKULU






Mbunge wa Ulyankulu, John Kadutu (CCM) ametishia kuzusha ‘vagi’ (vurugu) jimboni kwake kama Serikali haitawaondolea kero ya maji.
Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maji leo , Bungeni jijini Dodoma, Kadutu amesema Jimbo lake kwa muda mrefu limetengwa na halipewi kipaumbele huku wananchi wake wakitaabika kwa ukosefu wa maji.
Kadutu ambaye amezungumza kwa hisia, amesema yeye na wananchi wanakwenda kuziba Mto Malagalasi kwa sababu mradi wa Mto huo badala ya kuhudumia pia wananchi wa Ulyankulu, umeelekezwa Kaliua na Urambo mkoani Tabora.
“Mheshimiwa Waziri na wataalam mlioko hapa nyuma yangu hebu fanyeni mnavyoweza, je tutatengwa hadi lini?, sisi sio wakimbizi kama hamtaki kutupa tawala za mikoa tupeni maji, wataalam msikie tutaleta vagi hata wao hawatakanyaga huko,” amesema.


(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.