JINSI YA KUKABILIANA NA WIVU KWENYE MAPENZI





Unapopata hisia za wivu, jambo la kwanza la kufahamu ni kwamba bado hujaweza kujiamini ipasavyo. Hujaweza kujipenda mwenyewe. Tafuta msaada wa kitaalamu uweze kujiamini na kujipenda mwenyewe kwanza kabla ya kusubiri mtu mwingine akupende kwa kiasi unachotaka. Na kuna ukweli fulani kwamba ni mara chache unaweza kumbadilisha mwenzako. Kumbe kwa kutokujiamini na kujipenda, unajiwekea mazingira ya kuteseka unapoingia kwenye mahusiano. 

Kwa lugha rahisi kabisa, hisia za wivu maana yake ni kutokuamini watu. Una mashaka na tabia za watu. Unaamini uko sahihi, wengine wanakosea. Badilika. Tafuta msaada uweze kuwaamini watu. Itakusaidia kuepuka kuteseka kwa mambo yasiyokuwepo kwa sababu tu huwezi kuwaamini watu. Kutokuamini, ndiyo wivu wenyewe.

Ni kweli kuwa wakati mwingine hisia za wivu huwa hisia za hali iliyopo. Kwamba ni kweli yupo mtu wa tatu katika mahusiano yenu. Kama mwanadamu unajisikia vibaya. Lakini dawa si wivu wa kiwango cha kupambana na mshindani wako.  Katika mazingira hayo, wakati mwingine tatizo huwa ni wewe. Ndio. Huenda hujalipa gharama ya kumfanya mpenzi wako ajisikie kupendwa na kuthaminiwa. Huenda umemfanya ajisikie kutumika kama daraja la mtu kufikia malengo mengine ya kimaisha. Badilisha mtazamo wako. Tafuta msaada wa kukufanya ujisikie mwenye wajibu wa kuleta mabadiliko kwenye mahusiano yako. Wivu haukusaidii kutatua matatizo yako.

Wivu usikufanye upambane na mtu asiyehusika. Hasira ni kiburi. Hasira, tunaambiwa haijawahi kutenda haki. Itakugharimu kukarabati mahusiano kwa kuongeza duara la mapambano na mtu wa tatu. Pambana na mwenzi wako kwa kumpa haki yake. Kama una hakika analo tatizo la kuvutwa na vya nje, kabiliana naye abadilike. Tafuteni msaada wa kitaalam kushughulikia mahusiano yenu. Hamna haja ya kupambana na mtu wa tatu ambaye kimsingi mmemkaribisha wenyewe.

Wivu ni sumu mbaya katika mahusiano. Unapojisikia hatari ya kumpoteza mpenzi wako, unapojisikia unatumia nguvu nyingi kuliko anazotumia yeye, maana yake ni kwamba bado hujampenda. Ni hatari ya hisia zako, na za mwenzako. Unajeruhi hisia zao mara nyingi kwa jambo lisilokuwepo. Unajikuta unachukua hatua zinazoongeza majeraha hata baada ya kushughulikia tatizo lenu. Upendo wa kweli hauhesabu gharama. Upendo hauna masharti. Unapompenda mtu, hufikirii yeye anafanya nini. Na unapofanya hivyo, mara nyingi, unamsababisha kubadilika.

Kabla hujafanya maamuzi ya kuhusiana na mtu, jitathimini. Jichunguze mwenyewe kwanza. Je, unajiamini? Unaamini wengine? Unafikiri nini kuhusu kupenda na kupendwa? Je, mahusiano ni kulipa gharama au kutarajia kutendewa? Kama huna hakika, tafuta msaada ndipo uweze kuingia kwenye mahusiano. Vinginevyo, utamjeruhi huyo unayetaka kuhusiana nae, utajijeruhi mwenyewe, na zaidi, utajeruhi wengine. Kwa sababu wivu, imethibitika, ni jaribio la kumtumia umpendaye kudhihirisha ulivyo na mtazamo hasi nafsi yako mwenyewe. Ishughulikie.


(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.