Aunty Ezekiel Awavaa Wanaohoji Kuhusu Mpenzi wake




Staa wa Bongo movie, Aunt Ezekiel amewataka wanaofuatilia mahusiano yake kumwachia mwenyewe, huku akidai suala la yeye kuwa na wanaume aliowazidi umri kwake si tatizo. 
Aunt Ezekiel amesema amekuwa akikutana na maneno mengi, huku wengi wakidai amekuwa na tabia ya kutembea na wanaume wadogo kuliko umri wake, kitu ambacho kwake haoni tatizo, kwa kuwa wengi hawajui hayo ni maisha binafsi ya mtu. 
“Suala la mimi kutembea na wanaume wadogo sidhani kama linatakiwa liingiliwe, haya ni maisha binafsi ya mtu, najua kila mmoja ana aina ya maisha anayotaka aishi, nadhani sipaswi kuingiliwa katika hili zaidi ya watu kushabikia kile ninachofuata,”alisema Aunt. 
Kwa sasa inadaiwa staa huyo ameachana na baba wa mtoto wake, Mose Iyobo, ambaye ni mnenguaji wa lebo ya WCB, ambao walijaliwa kupata mtoto aitwaye Cookie.


(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.