USIOMBE MSAMAHA KWA KUKARIRI CHKUA UJUZI HAPA
Weka ubongo wako wazi, kuruhusu somo hili kichwani mwako, ambalo litakuwa hazina yako na mwongozo katika uhusiano wako.
Kitu kikubwa ukumbuke, kukosea ni kawaida. Inatokea kila siku katika maisha yetu, hilo litoshe kukupa umuhimu wa kufuatilia kwa makini somo hili. Karibu darasani marafiki.
JAMBO LA KWANZA
Tafakari ukubwa wa kosa;
Hapa tayari umeshagundua kwamba umemkosea mpenzi wako na ni kweli kwamba unaumizwa sana na kosa lako, lakini kwa ababu hujamwambia chochote, naye hana raha na wewe. Hana amani ya moyo.
Hapa unashauriwa kutulia na kutafakari ukubwa wa tatizo. Kufahamu ukubwa wa tatizo kutakupa muongozo mzuri sana wa jinsi ya kutatua tatizo hilo. Angalia ulimfanyia nini na kwa kiwango gani?
Mathalani unaweza kuwa ulimuudhi kwa ababu alikupigia simu zaidi ya mara kumi bila kupokea, akakasirika. Hili ni kosa dogo. Lakini yawezekana alikuta meseji ya mapenzi kwenye simu yako au alikufumania; Haya ni makosa makubwa. Tafakari na ujue ukubwa wa kosa lako.
JAMBO LA PILI
Jutia kwa moyo;
Hii ni kwa ajili yako wewe mwenyewe. Rafiki zangu, kutakuwa hakuna maana yoyote kuomba msamaha wa kinafiki au kuomba msamaha ili kumaliza mambo, kama msamaha wako haujatoka moyoni.
Ukiwa peke yako, jiaminishe kwamba umekosea na kwa hakika unahitaji kusamehewa.
Jutia ndani ya moyo wako, kwa dhati kabisa ukiwa na ahadi kwamba hutarudia tena. Hili ni zoezi la Kisaikolojia, ambalo litakusaidia baadaye wakati ukikutana na mpenzi wako kwa ajili ya kuomba msamaha.
JAMBO LA TATU
Mpe ukweli;
Omba kukutana naye. Yawezekana hata mawasiliano si mazuri sana, lakini hapa jitahidi kumuomba mkutane, ikishindikana, tumia mtu wa karibu sana na yeye. Omba kutoka naye kwa ajili ya kuzungumza.
Mweleze ukweli wa kosa lako, onesha jinsi linavyokutesa na kukusumbua. Usijaribu kuongea uongo wowote katika suala hili. Kuwa mkweli. Jutia kwa moyo, aone majuto yako usoni mwako.
Mwambie jinsi unavyoteseka na jinsi msivyo katika maelewano mazuri. Kauli yako ya ukweli, hisia zako wakati wa kuzungumza, ndivyo vitakavyokuweka katika mazingira mazuri ya kuweka mambo sawa.
JAMBO LA NNE
Ahidi kutorudia makosa;
Bila shaka, kama utakuwa umefuata taratibu zote hizo kwa umakini, uwezekano wa kusamehewa ni mkubwa sana. Hili ndiyo matarajio yangu, naamini hata wewe pia, lakini ili msamaha huo ukamilike, mhakikishie mpenzi wako kuwa hutaruidia tena.
Mwambie kwa kumaanisha, kwamba umegundua udhaifu wako na haupo tayari kumfanya tena asiwe na furaha. Hakuna uchawi ni maneno tu!
JAMBO LA MWISHO
Mfanyie kitu maalum;
Hapa unatakiwa kufanya kitu maalumu kwa ajili ya mpenzi wako, ukionesha kwamba umekubaliana na msamaha wake na mambo yameisha. Kitu utakachokifanya hapa utalinganisha na ukubwa wa kosa kama nilivyosema awali.
Mathalani unaweza kutoka naye na kwenda kulala naye hotelini, ukihakikisha unampa mahaba mazito kama shukrani kwake.
Yapo mengi ambayo unaweza kuyafanya kulingana na uwezo wako kifedha. Fanya vyovyote ili kosa lile lisahaulike moja kwa moja.
Yes! Kila kitu kipo mikononi mwako? Bado hujasamehewa tu? Labda awe tayari ana maamuzi mengine, vinginevyo hapo hapindui
(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA
KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
No comments: