SOMA KISA HIKI CHA KUSIKITISHA KISHA MPE USHAURI





SOMA KISA HIKI CHA KUSIKITISHA KISHA MPE USHAURI
MAMA HUYU AFANYE NINI ILI KUJIKWAMUA NA
MATATIZO ALIYOYAPATA.....
Mimi ni mama mwenye watoto 5 na ninaishi katika kijiji
kimoja huku Mkoani Lindi.Nimeolewa na mwanamke
mwenzangu ambaye nimemzalia watoto kutokana na mahari
aliyoitoa kwa bibi niliyekuwa naishi naye.Wazazi wangu
walifariki dunia nikiwa na umri wa miaka 7 tu ambapo
ililazimika kulelewa na bibi yangu mzaa mama.
Malezi ya huku kijijini kwetu siku zote siyo mazuri na hii ni
kutokana na hali duni ya maisha tuliyonayo.Kutokana na hilo
sikufanikiwa kwenda shule hata darasa moja.Badala yake
nikawa namsaidia bibi kazi za shamba na za pale
nyumbani.Baada ya kuvunja ungo,miezi kadhaa baadae bibi
aliniambia amenitafutia mtu wa kunioa hivyo nijiandae
kuingia katika ndoa.
Kutokana na desturi zetu hilo wala halikuwa jambo la
kushangaza kwangu.Siku moja baada ya bibi kupokea mahari
alikuja mama mmoja pale nyumbani kwa lengo la
kunichukua.Bibi aliniambia kuwa natakiwa niondoke na
mama huyo.Mimi nilidhani pengine kwa huyo mama ndio
nitamkuta mume wangu kumbe yeye ndio alikuwa
amenitolea mahari kwa lengo la kunioa.
Nilipofika kwake aliniambia anaishi peke yake na yeye ndio
mume wangu.Nilishangazwa sana na jambo hilo kwani
sikuwahi kusikia mahali popote pale kwa wanawake kuoana
wenyewe kwa wenyewe.Mama huyo aliniambia amenioa kwa
lengo la kumzalia watoto kwani yeye hakubahatika kupata
mtoto hata mmoja enzi za ujana wake.Nilizidi kubaki njia
panda nikijiuliza nitamzalia vipi watoto bila mwanaume.
Baada ya mwezi alikuja mwanaume mmoja pale nyumbani
na mama huyo akaniambia nilale naye mpaka nitakaponasa
ujauzito.Mwanaume huyo alinitumia kwa mwezi mzima na
baada ya hapo akaondoka zake.Kwa kweli nilinasa mimba na
baada ya miezi 9 nikajifungua mtoto wa kiume.Tuliendelea
na maisha hayo mpaka nilipofikisha mtoto wa 3 kila mmoja
na baba yake.Mama huyo aliniambia kuwa hao siyo watoto
wangu bali ni wake kwa kuwa amenilipia mahari na vile vile
huwa anawalipa wanaume wanaokuja kunipa ujauzito.
Vile vile alinitaka nimpe heshima zote anazostahili mume na
nilikuwa namwita mume wangu kama kawaida.Alinikataza
kabisa kuwa na urafiki na mtu yoyote pale kijijini bila hidhini
yake.Hata kwenda kumsalimia yule mama aliyenilea hakuta
kabisa.Niliendelea na tabu hizo mpaka nilipotimiza watoto
watano kwa wanaume tofauti tofauti.Watoto wangu
wanamwita yeye mama na mimi wananiita dada.Jambo hilo
linaniumiza sana.
Sasa hivi nimetoroka nipo kijiji kingine ila watoto wangu
wote wamebaki kwa yule mama.Nasikia kwamba
ananitafuta kila kona kwani alipotoa mahari alitaka nimzalie
watoto 10 na mimi nimezaa 5 tu na kuyoyoma zangu.Nataka
niwafuate watoto wangu lakini naogopa akinitia mbaroni si
nitakuwa tena mtumwa wake!Au niwaache watoto niendelee
na maisha yangu mengine?....
NAOMBENI USHAURI WENU.


(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.