Tulioko kwenye ndoa kukaribisha mashosti nyumbani wamzoee Mr ni kutengeneza bomu



Ukiwa kwenye ndoa mume ana sehemu yake katika maisha yako. Binadamu tukiwa social animals tunahitaji marafiki, wa kusaidiana nao katika kuongeza siku hapa dunuani. Ukiwa kwenye ndoa inabidi uwe na mipaka katika uhusiano wa mashost kumzoea mume wako.

Kwanza shost kuja nyumbani si busara. Nyumbani ni sehemu ya familia na privacy izingatiwe. Yale mambo ya kuanikana siri barabarani kuwa wakimaliza kula yule mwanaume ndiye muosha vyombo hayahusu.

Ikitokea shost amepata dharura inabidi aje kwako. Apige simu na uelewe sababu inayomleta. Kama mume yuko sebuleni anaangalia TV, mtake radhi aende chumbani japo kwa lisaa limoja, unaihitaji sebule. Akija shost msikilize, baada ya lisaa ulilomuahidi mume kwisha mtake radhi shoga kuwa muda wa kumsikiliza umekwisha, mengine mtayamaliza kwenye simu.

Kama watazoena wazoeane kwa kukutana ki vyao si chini ya pua yako.

(WAKUBWA TU 18+) JIFUNZE UFUNDI NA UTUNDU KATIKA MAPENZI UBORESHE MAHUSIANO YAKO PAKUA APP YA UFUNDI CHUMBANI , BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

No comments:

Theme images by imagedepotpro. Powered by Blogger.